Mkumbwa Jr
JF-Expert Member
- Mar 23, 2016
- 2,624
- 3,653
Prof.Ndalichako ninakupongeza kwa kazi unazofanya ingawaje nizautaalamu lakini zinamiongozo tele ya wanasiasa.
Changamoto zilizopo ndani ya wizara yako ni nyingi na yapo mambo lukuki ambayo huchangiwa na uzembe,ubinafsi,ubabe wa baadhi ya viongozi ndani ya kada husika,kufanya kazi kwa mazoea nk.Mkusanyiko wa yote hayo hupelekea matokeo mabovu katika ngazi zote.
Tukianza na changamotokubwa kulikozote niwakuu wa shule.
Hao ni miungu watu (baadhi yao sio wote)huamua na maafisa elimu na wakurugenzi ni lini wahame vituo na nivituo gani wanataka kwenda lengo kubwa nikugawana maslahi mfano fedha za uhamisho nk.Mkuu wa shule anakaa kwenye kituo miaka kumi hakuna mwanafunzi mwenye daraja la kwanza,lapili wala la tatu na hao wenye daraja la nne ni asilimia ndogo wengi ni SIFURI.
Wakiulizwa sababu za wanafunzi kufeli wanasema hakuna walimu wa sayansi,maabara.Swali ni Je hayo masomo yenye walimu tele wanafunzi wamefaulu kwa kiwango gani?
Haiwezekani mtu anajiita mkuu wa shule kwa miaka kibao na anasherehekea ziro kaziyake ni kuhudhuria vikao,kusahihisha mitihani,kula hela za viti na meza nk.Hawana uchungu na watoto,hawawajibiki kwa kuwasimamia vyema walio chini yao kwakua wao wanayomapungufu yasiyo hesabika.
Wakishauriwa wanasema ni wazoefu,wazoefu wa kutoa zero?
Mh.Ndalichako waelekeze wakurugenzi na maafisa elimu kote nchini yafuatayo,
.Wakuu wa shule wawe wanahamishwa kila baada ya muda
.Wakuu wa shule wasipendekeze majina ya wasaidizi wao
maana hao wasaidizi hawawi watu huru bali hues watumikishwaji na wasainishwaji cheki na mauzauza kibao
.Wakuu wa shule waliodumu kwa miaka zaidi ya sita katika nafasi zao kwenye shule husika na kuonekana hakuna ahueni kwenye matokeo kwakua na sifuri lukuki basi washushwe vyeo na wasibakie kwenye shule hizo maana hawana mbinu mbadala.
Wakurugenzi ambao hawaonekani kusimamia ubora wa elimu ishauri mamlaka yao iwatazame upya
Pia wanasiasa kama watendaji wa kata wasiingilie mambo ya kitaaluma bali kama kuna kero zifikishwe kwa maafisa elimu.Watendaji na waratibu elimu baadhi wanamihemko ya kisiasa kuliko utendaji
Wapo madiwani wenye njaa kama mchwa hata ujenzi wa choo,vibao vya shule,vifaa vya michezo wanataka wachukue tenda,wanunue vifaa na kusimamia wao eti nao nimaboss kwenye kada hiyo.HAPO SERIKALI IANGALIE UPYA MADIWANI WASISHIRIKI KAMA WASIMAMIZI WA WAKUU WA SHULE BALI WAKACHUKUE KERO NA KUZIFIKISHA SEHEMU HUSIKA AMBAPO NI HALMASHAURI.Ninasema hivyo kwani wapo madiwani ambao wanajifanya shule ni zao na walimu wanazisusa shule na hatimaye familia za wanafunzi kuonekana zinapoteza muda na hela,taifa kupata hasara
Haiwezekani mtu atoke kuchoma mkaa aje amshauri mkuu wa shule namna bora ya kuisimamia shule kwa kuja hadi paredi na kuwapa walimu maelekezo mbele ya wanafunzi,akitoka hapo akamfokee mganga/muuguzi hospitalini,mtendaji kata,HIYO SIO SAWA WATAALAMU WASIMAMIWE NA WATAALAMU NA SIO WAPIGA ZUMARI.Lengo nikuziponya kata au mitaa yote nchini
Tupa siasa pembeni fanyakazi,changamoto za rasilimali watu,vifaa,maslahi zitatue haraka uwezavyo.Jina lako halitasahaulika katika historia ya watumishi na viongozi bora,imara na walioleta mabadiliko chanya katika taifa hili.
Nimetimiza wajibu wangu kwa taifa langu