Kauli ya Ndalichako(kama kweli alisema hivyo) ya kwamba mwenye sifa ya kuingia chuo kikuu ni form six leaver tu, tena aliyefaulu, inavunja katiba ya nchi, sheria ya elimu ya mwaka 1978, Haki za binadamu, sheria za kimataifa(International laws) ambazo TZ ni mwanachama, Sera ya Elimu ya mwaka 2014, Ilani ya CCM(2015-2020), na miongozo mbalimbali ya elimu nchini.
Mimi na mwana CCM hai. Napingana kabisa na kauli hiyo, kwasababu inawanyima haki watoto wa masikini wanaosoma shule za kata kupata haki ya kusoma chuo kikuu. Je kijana huyu ata re-sit form 6 hadi lini? Kwa gharama ya nani? "Justice delayed is justice denied".
Tuangalie hali halisi na tuwe wakweli. Huku vijijini ktk shule za kata walimu wachache, maabara hakuna, vitabu hakuna, umeme hakuna, maji shida, matibabu duni, pesa kwaajili ya ada na michango mbalimbali shida, matatizo mengi ya kifamilia kwasababu ya umasikini, nk.
Hivyo ni vigumu sana vijana kufanya vizuri ktk mitahani yao. Sisi watu maskini equivalent qualification ya kuingia chuo kikuu ambayo ni diploma imetusaidia sana kuingia chuo kikuu.
Tunapomaliza form 4 au 6 kama tumefeli, huanza kusomea taaluma ya "kazi" kwa kiwango cha certificate au diploma ili tujiendeleze huku tukiwa kazini.
Kwahiyo, kauli yake hiyo imetoka kwenye kinywa cha "tajiri" anayeishi Masaki, asiyejua kuwa kuna masikini wengi ktk nchi hii, hasa vijiji.
Hiyo kauli ikiachwa itekelezwe, itakuwa vigumu sana kwa sisi masikini kusoma vyuo vikuu. Vyuo vikuu vitakuwa kwaajili ya watoto wa matajiri tu.
Na ikiwa hivyo masikini tutaenda kuipinga mahakamani. Tunapotoa kauli mbalimbali(executive orders) tuangalie hali halisi na haki za walio wengi, hasa masikini.
Kifanyike nini:
1. TCU/NACTE kuweka cut-off GPA ya mwenye diploma kuingia chuo kikuu.
2. NACTE/TCU kufuatilia ubora wa utoaji elimu ktk vyuo vya kati na vyuo vikuu.
3. Vyuo vinavyotoa elimu ya kati visipandishwe hovyo kuwa vyuo vikuu. Vyuo vya kati ni msaada mkubwa sana kwa vijana, hasa maskini vijijini.
4. Maamuzi/matamko mbalimbali,hasa yanayogusa haki na masilahi ya wengi yasitamkwe kwa mihemuko ya mtu moja(abuse of discretionaly powers),bali yawe ni tunda la maamuzi ya wengi/shirikishi(wadau, wataalamu na kamati mbalimbali ambazo zipo kisheria).
5. Uhuru wa mtu kuamua afikie malengo yake kwa njia ipi, ulindwe.
6. Kabla ya kutoa matamko tusome katiba ya nchi, sheria na sera mbalimbali ambazo zinagusa jambo hilo(Rule of Law).
7. Kutaka sifa na kujenga majina yetu mbele ya wateuzi, kusiwe chanzo cha kunyang'anya haki za masikini ambao hawana uwezo wa kujitetea.
Note: Ni kweli tunahitaji kuboresha elimu, lakini ktk kufanya hivyo tuzingatie katiba ya nchi, sheria ya elimu, sera ya elimu, maamuzi shirikisha, ilani/manifesto, kufanya tafiti kabla ya kutoa tamko.