GE2025 Nchimbi: Wana CCM wametangaza tarehe 29 Oktoba ni Samia Day

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea mwenza wa Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Emmanuel Nchimbi amesema Wana-CCM na Wakazi wa ilala wametangaza kuwa siku ya uchaguzi Oktoba 29 ni samia Day

Nchimbi amesema hayo Leo Oktoba 1, 2025 akiwa katika mkutano wa kampeni maeneo ya Machinga Complex jimbo la ilala Jijini Dar es salaam Katika muendelezo wa kunadi sera za chama cha mapinduzi pamoja na kumuombea kura Rais Samia Suluhu Hassani, wabunge na madiwani

Mbali na hayo Dkt Nchimbi amempongeza Mgombea ubunge wa Jimbo la ilala Mhe Azzan Zungu katika kipindi alichotumikia ndani ya CCM hasa nafasi yake ya ubunge katika jimbo hilo pamoja na kutambua mchango wake ndani ya Chama

Aidha Dkt Nchimbi amewasilisha Salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wakazi wa ilala.
Your browser is not able to display this video.
 
 
Huuu mvutano nimzuri sana
Huku tunatiki
Huku tunaandamana
Huku samia day
Mnauhakika mnao polisi wa kutosha kusimamia yote hayo
 
Atakuwa amemaanisha ni kilele cha siku ya maigizo bila shaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…