Nchimbi Amridhi Lowasa Uvccm.

Nchimbi Amridhi Lowasa Uvccm.

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,426
Reaction score
3,309
BARAZA Kuu la Umoja wa Vijana
wa CCM (UVCCM), jana
lilitangaza majina mapya ya
Wajumbe wa Baraza la
Wadhamini, huku likiweka
kando jina la Waziri Mkuu wa
zamani, Edward Lowassa.
Akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kikao cha
baraza hilo kilichofanyika mjini
Dodoma mwishoni mwa wiki,
Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin
Shigela alisema nafasi ya
Lowassa aliyekuwa Mwenyekiti
kwa miaka 10, inachukuliwa na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
(pichani).
Shigella aliwataja wajumbe
wengine walioteuliwa kuwa ni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge),
William Lukuvi, Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Profesa Anna Tibaijuka,
Naibu Waziri wa Fedha, Janeth
Mbene, Waziri wa Nchi (Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais
Zanzibar), Mohamed Abood,
Waziri asiye na Wizara
Maalumu Zanzibar, Machano
Othman Said na Mbunge wa
Kikwajuni Hamad Masauni.
Shigela alisema katika kuteua
wajumbe hao, kikao hicho cha
UVCCM kilizingatia uwezo wao
katika ushawishi na
kuwaunganisha vijana “bila ya
kuwapo kwa makundi.” Hata
hivyo, hakufafanua maana ya
makundi hayo.
Kuondolewa kwa jina la Lowassa
ni pigo jingine kwa mwanasiasa
huyo ambaye amekuwa akitajwa
kuwa miongoni mwa wanaotaka
kuwania urais kupitia CCM
katika Uchaguzi Mkuu ujao. Jina
lake pia halikupendekezwa
miongoni mwa wagombea wa
ujumbe wa Kamati Kuu (CC) ya
CCM katika uchaguzi uliofanyika
wiki iliyopita.
Lowassa alikuwa ameanza
kuibuka tena kisiasa kutokana
na kambi yake kupata ushindi
mkubwa katika mchakato wa
chaguzi za ndani za chama hicho
zilizowaingiza wafuasi wake
wengi kwenye nafasi za Ujumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa
(NEC) na katika jumuiya za
chama hicho.
Wajumbe wengine walioachwa
ni Nazir Karamagi, Dk Mary
Nagu, Yusufu Ame Yusufu na
Said Abuu.
Kwa upande wa Dk Nchimbi,
nyota yake ya kisiasa
inaonekana kung’ara kiasi cha
kuanza kutajwa kuwa mmoja wa
makada wa CCM wanaoweza
kuteuliwa kumrithi Rais Jakaya
Kikwete kupitia chama hicho
katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Katika uchaguzi huo wa Kamati
Kuu ya CCM, Dk Nchimbi
alichaguliwa kuwa mjumbe
pamoja na wenzake sita kutoka
Tanzania Bara, baada ya
kupendekezwa na Rais Kikwete
kuwania nafasi hiyo.
Itakumbukwa kwamba miaka 10
iliyopita, Dk Nchimbi katika
kipindi chake cha pili cha
Uenyekiti wa UVCCM, ndiye
aliyependekeza jina la Lowassa
kuwa mwenyekiti wa baraza
hilo, mpango ambao ulipingwa
na baadhi ya wanachama
wakiongozwa na Nape Nnauye
ambaye hivi sasa ni Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM.
Nape alifikia hatua ya
kufukuzwa ndani ya jumuiya
hiyo na hata alipotaka kukata
rufaa alijibiwa na aliyekuwa
Katibu Mkuu wa CCM, wakati
huo Yusuph Makamba kwamba
asingeweza kurejeshwa katika
jumuiya hiyo, hata kama
angekata rufaa mbinguni.
Kikao hicho cha Baraza Kuu la
UVCCM, pia kiliteua wajumbe wa
Kamati ya Utekelezaji ambao ni
Daud Njalu, Reuben Sixtus, Seki
Kasuga, Amina Mkalipa na
Mariamu Chaurembo ambao
wanaingia kupitia Bara. Kwa
upande wa Zanzibar waliopata
nafasi hizo ni Shaka H Shaka,
Bakari Vuai, Nadra Mohamed,
Viwe Khamisi na Ali Nasoro.
 
Back
Top Bottom