Nchi zilizoendelea nazo ziliendekeza uwekezaji kutoka nje

Mzux

Member
Jan 19, 2013
29
7
Hili ni swali ambalo huwa nakaa najiuliza sana kila ninapoona juhudi za serikali kutafuta wageni na kuwahimiza kuwekeza kwenye kila sekta.

Ninapokuja kwenye sekta ya kilimo ndipo najiuliza zaidi. Hivi serikali inashindwa kuweka mikakati ya kuwasaidia watu wake waweza kufanya kilimo kiasi cha kuhimiza wawekezaji wa nje hata kwenye hii sekta ambayo binafsi naamini unahitajika ubunifu tu na mikakati ya kuwawekea ha wananchi? Nionavyo mimi kuhimiza wawekezaji kutoka nje kwenye sekta ya kilimo ni ukosefu tu wa ubunifu na fikra kwa viongozi wetu.

Kila nikitafakari nakumbuka nchi ya China chini ya kiongozi wao Mao na jitihada zao kwenye mapinduzi ya kijani. Watu waliweza kusaidiwa na kuzalisha wenyewe. Sisi tunaendekeza wawekezaji. Je mwisho wa siku wananchi walio wengi watakuwa wanafanya nini kama si kuendelea kuzalisha tu kwa mazoea.

Nadhani ifikie hatua serikali itimie wataalamu wanaozalishw kuwasaidia wananchi wake. Serikali itambue kuwa ina jukumu la kuwasaidia wananchi wake kuwapa ujuzi ili washiriki katika uchumi wa nchi na kujikwamua na isiishie kuona ina jukumu la kuita tu wawekezaji.

Tanzania ina rasilimali nzuri ya ardhi ambayo kama serikali itaweza mikakati ya kuwasaidia watu wake hakika maendeleo yatapatikana. Tukumbuke kuwa maendeleo ya nchi yanaanza kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja.

Tanzania inahitaji viongozi wabunifu sio wale wanaodhani kuwa jukumu lao kuu ni kufanya teuzi za watendakazi tu.
 
Wawekezaji wa ndani kina Mbowe si unasikia kinacho wapata!? KWa ujumla hua ninadhani hivi; sisi watu weusi tunalo tatizo kubwa zaidi kuliko hi RANGI yetu. Mgeni akizurumu KODI ni sawa au sometimes tunaweza hata kumsamehe KODI but wewe fungua tu kioski cha kuuza SODA; siku ile unajaza tu soda kwa duka/kioski chako kabla hata mteja wa kwanza hajanunua SODA hakikisha TRA umeisha waona; kwa maneno mengine KODI iwepo kwenye bajeti ya MTAJI wako.
 
Back
Top Bottom