Nchi za magharibi ni zipi?


Thanks mkuu.
 

nashukuru kwa muongozo wako!! kuna hili ten...
kwa nini nchi kama Tanzania inaitwa nchi dunia ya tatu "third world country"?? je kuna dunia tatu?? na je "second world countries" ni zipi?
 
je na mtu aliye location tofauti na yetu nae atasema ni nchi za magharibi?

Kwani ukiwa Asia Afrika inabadilika inakuwa east au kaskazini?

ramani ya dunia si inabaki kuwa vilevile NEWS.
 

Ngoja nami nijaribu kukujibu,

Kwanza unaujua mstari wa Longitude kuu?? Iko mistari mingi lakini mi nazungumzia ule Mkuu wenye Nyuzi 0. Sasa Ule ni imaginary line ulioigawa dunia. Unatoka kaskazini (juu) hadi kusini (chini) .

Sasa basi ukichora ule mstari, chochote kilichoko kulia ni kiko mashariki, na chochote kilichoko kushoto kiko magharabi. Assumption ni kua umeelekea kaskazini.

Sasa Nchi za magharibi zinatokea kushoto kwa ule mstari. Labda tatizo lije kwamba why mfano Morocco haipo kwenye "Nchi za Magharibi" wakati yenyewe ipo Kushoto kwa Longitude kuu, hapo wataendelea wengine!!
 
Hii ilitokana na misimamo ya siasa za kibepari na kikomunist wale wakomunist waliwaita wenzao "wamagharibi" and viceversa,taabu ikaja watu wa 'dunia ya tatu "ambao hatuko mashariki wala magharibi nasi tukazibeba nchi za ulaya zote na america "za magharibi" ila kiukweli jina hili ni zao la vita baridi kati ya wakomunisti na mabepari(mtizamo wangu ruksa kusahihishwa)
 

kaka hiyo East na West ina reference ya nchi za Ulaya, labda inawezekan reference ilikuwa pale german wakati vita ya Hitler inaisha na ndio berlin ikagawanya pale na kuwa East german iliyokuwa na Urusi na kisha USSR na upande wa west ilyokuwa na Uingerza, ufaranza na Marekania(japo yeye sio wa Europa) na ndio kukawa na East na West Europa,
kutokana na misimamo ya kisias ya wakati huo, labda mpaka sasa nchi za West ziliendelea sanamkiuchumi kutokana na mfumo wao wa sias walikuwa wakiufat(Ubepari) kulinganisha na siasa za kicomunist za Russia na wenzie (yugoslavia, Poland, East garnam nk)

Unaposea nchi za Magharibi unakwa na geographical reference ya Europa probably kutokea German

Cc😡Mwambojoke
 


Kaka Shakiri unaweza usiwe sahihi sana hapo unaposema kila kilicho kulia ya Longitudo 0 ni Mashariki au kushoto ni magharibi, kwa maaa hata kitu kilichokuwa kulia ya Longutudo 0 bado kinakuwa na Mashariki na Magharibi, na kilichokua kushoto pia kina Magharibi na Mashariki

Tanzania iko kulia ya huo mstari lakini Tanzania ina Mashariki na Magharibi
 

Kwenye miaka ya 1400 Wareno walikuwa wanatafuta njia ya kwenda India kutafuta viungo(Spices) njia waliokuwa wanaitumia mwanzo ilikuwa ina vita sana, hivyo safari ya kwanza walipotoka waliingia Bahari kuu ili wapate upepo wa kuwaleta nchi kavu lakini walipotea na kujikuwa wakitokea Brazil, safari ya Pili waliamua watembee na ufukwe, pwani kwa pwani, hivyo walianzia na pwani ya Africa Magharibi na wakaweka reference yao Angola na walipofika South Africa ndio wakaona bahari mbili zinaungana, bahari ya Atlantic na hii Indian ocean ( kabla hawajaibatiza jina hilo) hapomsouth Africa ndipp walipopaita Cape of Good hope ( rasi ya matumaini) kutoka hapo wakafika Mozambique na wakafanya reference kamaile ya Angola,

walipofika Mozambique walianza kushaangaa na mivement ya biashara hasa zile za Sofara zilizokuwa zinaendeshwa na waarabu, na kutoka hapo walipofika Kilwa walikuwa ni nchi kubwa iliyoendelea sana na kuna vyombo vingi vya usafiri wa majini na ndipo walipowauliza hao mabaharia wa Kiarabu njia ya kwenda India maana sasa hawakuwa na haja ya kusafiri along the coast iliwapasa kuingia deep sea mpka India

Waarabu ndio,waliowaonyesha njia ya kwenda India na muda muhafaka( kutegemea na Upepo Kaskazi na Kusi)

hivyo Wareno ndio wakainote kwa hiyo ndio Bahari yamkwenda India, Way to India,

kumbuka Wareno ndio waliotoa majina ya Bahari zote kubwa, kila walipofiaka walikuwa wanadocument na kuweka kwenye ramani zao,za kwanza za Dunia, hivyo hilo jima Bahari ya Himdi sio la leo na na ni ngumu kulinadilisha
 
TUnaposema nchi za magharibi zaidi ni ile ideology waliokuwa nayo na huwa haimaanishi sana kijiografia....The western ideology hata kama upo mashariki ukiwa unafuata western ideology utaitwa mmagharibi....stuka...
 
TUnaposema nchi za magharibi zaidi ni ile ideology waliokuwa nayo na huwa haimaanishi sana kijiografia....The western ideology hata kama upo mashariki ukiwa unafuata western ideology utaitwa mmagharibi....stuka...
 
TUnaposema nchi za magharibi zaidi ni ile ideology waliokuwa nayo na huwa haimaanishi sana kijiografia....The western ideology hata kama upo mashariki ukiwa unafuata western ideology utaitwa mmagharibi....stuka...

Hiyo imekuja baadae sana, wakati wa NATO na WARSAW, ilikuwa huwezi kuwa East na ukawa Bepari, au West na ukawa Mkomunist, kwa sasa Yes
 
Mi naona kama watu wa Dar wanavyowaita wenzao wanaotoka nje ya Dar ni wa mikoani,kwani magharibi ya marekani ni wapi????????? au magharibi ya ulaya ni wapi????????
 
Mkuu Kituko: inawezekana ukawa unachanganya, ila ukija kwenye suala la kijiografia ni kweli kabisa kuna nchi za Ulaya Magharibi na Ulaya Mashariki (hizo zipo kabisa na wala si utani na haziangalii uchumi,maendeleo ama umaskini) hizi ni kama Afrika mashariki na Afrika Magharibi, kusini, n.k., yaani hii unaangalia kabisa jua linachomoza wapi na kuzama wapi. Ukiangalia Marekani ipo Magharibi ya Dunia "kijiografia na ipo bara la Amerika kaskazini" na haipo ulaya (europe).

Nchi zilizopo Ulaya Magharibi ni - kijiografia: "United Kingdom, France, Netherlands, Belgium, Luxembourg, Germany, Italy, Ireland, Denmark, Norway, Iceland, Sweden, Finland, Austria,nk" Marekani kwa maana ya USA haimo.
Na nchi za Ulaya Mashariki Kijiografia: Russia, Czech Republic, Poland, Hungary,Romania,Moldova,Croatia,Lithuania, Latvia, Estonia,Slovenia,Slovakia,Bulgaria,Ukraine, Belarus,Serbia,Montenegro, Bosnia na Herzegovina,Albania, Kosovo, na Macedonia".
Japo nakubaliana na wewe kuwa hapo mwanzo kulikuwa na uhusiano mkubwa kabisa kuwa hizo pande mbili (Ulaya Magharibi na Mashariki) zilitokana na habari za ubepari na ujamaa (ukomunisti) ambapo utakuta nchi nyingi za ulaya Mashariki zilikuwa ni waumini wa Ukomunisti - chini ya iliyokuwa USSR na upande wa pili nchi za ulaya magharibi zilikuwa na waumini wa ubepari chini ya Uingereza, ujerumani (magharibi).
Lakini kwa kumalizia ni kuwa Ulaya Magharibi na Mashariki tofauti yao ni kijiografia zaidi kuliko kimaendeleo ama mfumo wa kisiasa.

 
Dhana hii ilianzia katika nchi za kiarabu ambapo walikuwa wakiziita nchi zote zilizo magharibi yao MAGHREB kutokana na mila kukinzana hasa kutokana na watu walio kuwa wakiishi mji wa MAGHREB kule MOROCCO kupenda sana maisha ya anasa tofauti na taratibu za maandiko...

 
Mkuu Nakubaliana na wewe, japo suala hili linajichanganya na masuala ya kijiografia pia, ila chimbuko la nchi za ulaya magharibi linatokana na masuala ya vita baridi, kwamba Ulaya Magharibi ni nchi zilizokaa kijiografia upate wa magharibi mwa ulaya (ukweli kabisa), ila baada ya vita II ya dunia kukawa na pande mbili - kibepari (Ulaya Magharibi) na Mshirika wao Marekani (marekani kijiografia hayupo ulaya) na upande wa pili Wakomunist - Ulaya Mashariki - chini ya iliyokuwa USSR na nchi hizi nyingi zipo mashariki mwa ulaya.

Na sie akina hohe hahe tukaanzisha block yetu: nchi zisizo fungamana na upande wowote (sisi hatujakaa kijiografia sana, tupo kila upande tumesambaa) - tulikuwa hatufungamani na upande wa Mashariki wala magharibi mwa ulaya (kiuchumi), -block yetu ilikaa kimaslahi zaidi ili tusipate shinikizo kutoka magharibi ama mashariki, tulikuwa tunakula na kipofu, mwisho wa hayo yote tumeishia kuitwa nchi za kusini
 
Kiongozi: Dunia ya tatu haimanishi sayari tatu ila suala bado linaibuka kwenye mambo hayohayo ya maendeleo,kiuchumi,kisiasa, kijamii, nk. jamaa wana vigezo vyao vya kubainisha kuwa wewe sasa upo dunia ya kwanza (umeendelea sana), dunia ya pili (umeendelea pia),dunia ya Tatu (Mungu wangu angalia),Dunia ya nne kama ipo basi (wewe upo hoi sana Mungu tafadhali saidia), ila yote haya yanatokana na suala la maendeleo katika nyanja mbalimbali,
hebu jaribu kupitia hizi links
Countries of the Third World - Nations Online Project
First, Second, and Third World - Nations Online Project
#20. Uganda - TheRichest
Third World - Wikipedia, the free encyclopedia

nashukuru kwa muongozo wako!! kuna hili ten...
 

Kaka nimekupata, lakini nadhani unajichanganya kidogo

sehemu yoyote ya Dunia utakayosimama lazima itakuwa na East, West, Sud na Nord, sasa kwa hizo nchi ulizozicategorize kama za East na West hapo kwenye bandiko lako juu, zingine zinaonekana kabisa zipo tofauti kigeographia kama unavyosema, mfano hebu linganisha Poland au Czhecslovacia na nchi kama Sweden ama Finland

kwenye Bandiko lako unaziweka Poland na Czech kama ziko East Kigeographia na Sweden na Finland kama West Kigeographia wakati sio kweli, Poland na Czech ziko Magahribi ya Sweden na Finland, kwa maana Nyingine Sweden na Finland ziko East zaidi ya Poland na Czech

Hivyo East Europa na West Europa pamoja na kuangalia Geopgraphy kwa uchache wake, kigezo kikubwa kilikuwa ni political wings, Capitalist West na Socialist/Communist East
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…