Afrika tuna vipaji vya soka, tatizo letu pia ni UMASKINI ambao mwisho wa siku unasababisha wachezaji wetu wakose uzalendo. Na hii ni kwa baadhi ya mataifa ya Afrika, sio yote. Tunaweka mbele maslahi kuliko utaifa. Tumeona mifano ya timu za Cameroon, Nigeria, na Ghana mwaka huu wa kombe la dunia, kambi zao zimegubikwa na skendo za utovu wa nidhamu na migomo inayotokana na tutolipwa posho zao (umaskini). Utovu wa nidhamu ni kiashiria kwamba nilikuwaga maskini ila sasa nina power, hauwezi niambia kitu, kama walivyofanya kina Muntari na Boateng. Kina Drogba/ Etoo na wenzao mwanzo walikuwa maskini, sasa hivi wamesharidhika kifedha hivyo hamna tena ari ya kuchezea timu ya taifa, hii inaturudisha tena kwenye umaskini maana umaskini umemfanya apigane kisha afanikiwe na baada ya kupata alichotaka, hamna uzalendo tena. Nayapenda sana mataifa ya Afrika ya Kaskazini, inapokuja kwenye michezo, ni uzalendo kwenda mbele, wako tayari ata "kudanganya" ili ushindi upatikane. Mataifa yaliyoendelea kisoka ulimwenguni kama Spain, Ujerumani nk wachezaji wao wanalipwa mabilioni ya pesa na bado yuko tayari atoke damu uwanjani kwa ajili ya jezi ya taifa. Tunaitaji kujifunza toka kwa wenzetu. Upande wa makocha wa kigeni, nasapoti kuwa na makocha wa kigeni sababu wanatuletea mbinu tofauti za kimchezo. Ila pia endapo wazawa watapewa fursa na kuwezeshwa nina uhakika wataweza. Hivyo basi ni suala la sisi kujifunza na kutambua wapi tunakosea. Huenda labda inapokuja suala la wachezaji na nchi zetu kutokufanya vizuri ni suala la muda. Labda bado hatujapata "uhuru", hivyo basi "uhuru" tutaupata na nina uhakika ipo siku tutafanikiwa na kufika huko tunapotaka kwenda.