Nchi yetu inahitaji Viongozi na sio Watawala

Govt

Member
Oct 16, 2013
6
2
Ifahamike kwamba hivi karibuni nchi yetu imeingia kwenye sura mpya ya uongozi wenye mfano wa mabavu au kwa lugha nyingine udikteta!

Watawala mara nyingi ni waonevu na wanatumia nguvu nyingi kufiksha madaraka yao, hufanya mambo kama vile madaraka yao hayatokani na wananchi, wanakandamiza uhuru wa kujieleza, habari n.k hupenda kusikiwa wao tu!

Tunataka viongozi ambao wao ni mfano wa maisha halisi ya wale wanaowaongoza, wenye kujali utu, maisha ya watu, na wenye hofu ya Mungu.

Tusijidanganye kwamba kuwanyanyasa watu kutainua nchi hii! La hasha, nchi ni yetu sote na tutaijenga sote!
 
Back
Top Bottom