Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,315
- 38,454
Niliposikia kwa Mara ya kwanza kauli kwamba "kuna watu wanaishi kama malaika, ni lazima tuwashushe waishi kama Mashetani" nikajiuliza sijui kama tafsiri ya maneno haya inaeleweka sawasawa. Kwa tafsiri hii tulikuwa tunaambiwa kwamba nchi yetu imejaa Mashetani ilhali kuna watu wachache wanaishi kama malaika wakati na wao pia ni mashetani ama wanastahili kuishi kishetani.
Lakini pia funzo kuu tunalolipata kwenye matamshi haya, ni kuwa kati yetu ama tunaye shetani Mkuu anayeweza kushindana na nguvu inayowafanya watu kuwa Malaika na hivyo kwa kutumia nguvu aliyo nayo atawarudhisha watu hao ambao ni watu wake kwenye uasili wao, yaani Ushetani!!
Yawezekana pia tuna "Mungu" ambaye kwa uasili wake anazo nguvu za kumshinda shetani kwa kuwa yeye ndiye "Muumba wa yote" na vyote "vinatoka kwake" na hata shetani ni matokeo ya "Uumbaji wake". Iwavyo kwa vyovyote vile kauli ile inathibitisha au kuashiria kuwa Tanzania ni nchi wanayoishi mashetani!!
Lakini cha ajabu ni kuwa nchi hii ambayo imejaa mashetani na mashetani wachache wanaotaka kuishi kama malaika, bado wananchi wake wanaamini kuwa iko siku nchi yetu itageuka kuwa Paradiso badala ya Jehanam!
Kuna watu wanataka Tanzania iwe na viongozi waadilifu na wacha Mungu ilhali mchakato wenyewe wa kuwapata viongozi hao unaongozwa na vitendo vya Rushwa, kuminywa kwa haki za Baadhi ya wagombea, vitisho, ulaghai,uibaji kura,uchakachuzi wa matokeo na kila aina ya Ghiliba kwenye uchaguzi!!
Kuna watu wanataka Tanzania iwe ya viwanda wakati walioua viwanda vilivyokuwepo ndiyo hao hao kwa ushetani wao walijiuzia viwanda hivyo pamoja na rasirimali zake kwa bei ya kutupa na mpaka leo bado wapo kwenye ngazi za uongozi katika taifa letu na hawajachukuliwa hatua yoyote ile. Walioua viwanda ndiyo hao hao eti leo wameshika mkononi ramani ya Tanzania mpya yenye viwanda!!
Wapo wanaotamani tuwe na viwango vya juu sana katika elimu yetu, lakini hawajali Mwalimu moja kufundisha wanafunzi 100 darasani badala ya 45 inavyotakikana tena wakiwa wamekaa chini sakafuni. Shule haina choo, haina Maktaba wala Maabara (sizungumzii majengo), walimu wachache, wanafuzi wanatembea hadi kilomita 10 ili kufika shule, lakini bado tunataka matokeo makubwa sasa!!Mifano ni mingi ya tunaotamani Tanzania iwe kama peponi wakati sisi wenyewe ni mashetani.
Ole wako unayetamani kuishi kama malaika!!