Nchi ya Burkina Faso imeanza maombolezo ya siku 3 ya kitaifa, baada ya kuuawa kwa raia 38

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Nchi ya Burkina Faso imeanza maombolezo ya siku 3 ya kitaifa, baada ya kuuawa kwa raia 38 katika shambulio la kushtukiza lililotekelezwa na wanajihadi wa kiislamu kaskazini mwa nchi hiyo.

Akihutubia wananchi kupitia televisheni, rais wa nchi hiyo, Roch Marc Christian Kabore, amesema kilichotokea ni pigo kwa taifa na kuwataka wananchi kuungana kuhakikisha wanayashinda makundi ya kijihadi.

Kwa miezi kadhaa sasa nchi ya Burkina Faso inashuhudia mfululizo wa mashambulizi dhidi ya wanajeshi na raia kwenye maeneo ya Kaskazini ambako inapakana na nchi za Nigeria, Niger na Mali.

Rais wa Burkina Faso amelitaja shambulio hilo dhidi ya msafara wa magari ya wafanyakazi wa kampuni ya madini ya Semafo, kama uhalifu wa hali ya juu, lililotekelezwa na watu wenye silaha wasiojulikana. "Vitendo hivi viovu vinakumbusha enzi zilizopita, ambavyo vinalenga kuzua hofu kwa wananchi na kuhatariha demokrasia.
 
Mbona mnajichanganya nyinyi viumbe.
Huko juu umesema waislamu lkn mwisho umesema wasiojulikana.
Mbona mnafeli kila siku kuuchafua uislamu lkn hamkomi.
Acheni blaablaa
 
Back
Top Bottom