Nchi ipi tajiri kama Tanzania?

Nchi ipi tajiri kama Tanzania?

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,286
Reaction score
6,729
Kumekuwa na maneno ya kejeli na kebehi kwa Rais Magufuli kutokana na hatua zake anazochukua kulinda na kusimamia rasimali za taifa.

Ni kweli kabisa Tanzania ni moja ya nchi duniani zilizo na utajiri usiopimika, ambao ukisimamiwa vizuri, wananchi watakuwa matajiri kuliko wale wa nchi za Kiarabu, ambao wanategemea tu mafuta.

Nitoe mifano michache tu ya utajiri wa nchi hii kwa kilimo, ufugaji, utalii, uchimbaji madini, uzalishaji wa nishati, nk:
1) Ardhi yenye rutuba kwenye mabonde ya mito mikubwa isiyopungua saba:- Pangani, Rufiji, Mara, Kagera, Ruvu, Wami, Great Ruaha, Ulanga, Ruvuma, Rufiji, Malagalasi, nk

2) Maziwa ya maji baridi:- Tanganyika, Victoria, Nyasa, Manyara, Eyasi, Rukwa, NayronJipe, Chala, Babati, Duliti-See, nk

3) Ukanda wa bahari ya Hindi wenye urefu wa 1,424km

4) Mbuga zenye wanyama wa kila aina:- Arusha, Mkomazi, Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro, Ziwa Manyara, Serengeti, Tarangire, Gombe, Katavi, Mahale, Rubondo, Saanane, Kitulo, Mikumi, Ruaha,Milima ya Udzungwa, Sadani, nk.

5) Gasi, mafuta na aina mbalimbali za madini kama vile ya
(i)viwandani, km Diamond (Almasi), Gold (Dhahabu), Copper (Shaba), Tanzanite, Ruby, Iron (Chuma), Soda ash, Salt (Chumvi), Limestone (Chokaa), Gypsum, Gravel (Changarawe), Sand (Mchanga), Graphite, nk
(ii) Nishati km , Coal (Makaa ya mawe), na Uranium.

6) Zaidi ya asilimia 10 (10%) ya eneo lenye uwezo wa kuzalisha nishati ya umeme wa jua na upepo, ukubwa ambao ni sawa na taifa la Malawi, kiwango kama cha Hispania lakini zaidi ya jimbo la California, Marekani. Kwa mfano: ukanda wa kati (Mkoa wa Dodoma na Singida); ukanda wa kasikazini mashariki (Mkoa wa Kilimanjaro)

Hivi kwa utajiri wote huo, ni halali nchi iendelee kuwa omba omba! Kama alivosema leo Rais, akiwapa vyeti wanakamati ya makinikia, Tanzania imekuwa ikitowa misaada (donate) kwa ujinga na unyonge wetu, kumbe tunaibiwa.

Lakini viongozi wa upinzani, na mbeleko zao humu jamvini wako mbele kutetea na kulinda unyonge wao kwa kuwapigia mabwana zao.

NI AIBU kwao. Ifikapo 2020, wapinzani wataweza kweli kusimama majukwaani kujibu maswali ya Watanzania, kuhusu kauli na matendo yao?

Nawasilisha.

Cc Paskali, Mzee Mwanakijiji, Jingalao
 
Uzalendo ni mzuri xn, lkn kweny ukwel usibadili. Cjasoma post yako yote, unamaanisha hkn nchi yenye utajiri kama Tanzania hp Dunia au?
 
Kumekuwa na maneno ya kejeli na kebehi kwa Rais Magufuli kutokana na hatua zake anazochukua kulinda na kusimamia rasimali za taifa.

Mkuu sidhani ni kweli kwamba kuna kejeli kwa raisi kuhusu kulinda rasilimali za taifa. Kejeli mara nyingi ni JINSI raisi anavyofanya maamuzi katka kulinda rasilimali za taifa. Ndio maana kina Tundu Lissu walisema haya mambo ya kulinda rasilimal za taifa waliyapigania kabla hata Magufuli hajawa waziri, na kwamba wao wana tatizo na namna ya Magufuli anavyofanya maamuzi kulinda rasilimali zetu, kwamba anafanya maamuzi ambayo yanaweza yakatuumiza, japo kiushabiki tunayaona mazuri.

Kwa mfano, hili la Acasia la 50/50, japo ni mafanikio kwetu, lakini tayari investor wengi wamelielewa vibaya mno, na wengi wameanza ku-cancel mipango yao ya investments Tanzania. Kimsingi kile kinachoitwa investment environment in Tanzania inaonwa kuwa mbaya sana.

Kwa hiyo lengo la Raisi Magufuli ni nzuri sana, lakini namna ya utelekezaji wa malengo yake mazuri (good intentions) inatia shaka sana kwa long term benefits za Tanzania.
 
Haya sawa... Swali kwako, kwanini hii nchi yako pamoja na huo utajiri ulioorodhesha hapo lakini bado ni masikini, iko kwenye daraja ya dunia ya tatu na sehemu kubwa ya bajeti yenu mtategemea wafadhiri, zaidi ya 70% ya wanainchi wake wanaishi kwenye ufukara uliotopea na kikubwa zaidi mna miaka zaidi ya 55 tangu mpate Uhuru?
 
Hoja zako ni sahihi kabisa ila hilo la wawekezaji kusita, ni uamuzi wa mwekezaji mwenyewe, uamuzi ambao haupunguzi chochote katika adhima ya taifa kulinda rasmali zake. Kwa mfano, kutokuwekeza kwenye madini, ambayo tangu wamechimba taifa alijapata haki yake stahili, badala yaka hasara ya uharibifu wa mazingira na afya ya wanavijiji jirani na machimbo.

Pia hilo dai kuwa namna ya utelekezaji wake una walakini, wapinzani hawajatoa utekelezaji mbadala wanaoamini ni sahihi. Kama umemsikiliza Rais leo, sheria ya madini ilibadilishwa kwa hati ya dharura, kutokana na ripoti za kamati mbili za makanikia na za bunge. Kamati ya majadiliano imetumia sheria mpya ya madini kujenga hoja zilizozaa makubaliano aliyoyainisha Prof Kabudi.

Yote hayo yamefanyika kuitikia kilio cha upinzani kuhusu usimamizi mbovu na dhaifu wa rasmali za taifa, hususani madini. Wapi Rais ameteleza?
 
Haya sawa... Swali kwako, kwanini hii nchi yako pamoja na huo utajiri ulioorodhesha hapo lakini bado ni masikini, iko kwenye daraja ya dunia ya tatu na sehemu kubwa ya bajeti yenu mtategemea wafadhiri, zaidi ya 70% ya wanainchi wake wanaishi kwenye ufukara uliotopea na kikubwa zaidi mna miaka zaidi ya 55 tangu mpate Uhuru?
Nchi ilikosa uongozi bora. Uongozi wa sasa angalau una uthubutu na ujasiri. Unatekeleza ahadi kwa vitendo
 
Mkuu kazi ya upinzani ni kuibua hoja na kazi ya serekali ni kujibu hoja sasa kama sio upinzani tungejuaje kuwa tushalizwa na Richmond
tatizo ni chama cha ccm kutuingiza mkenge kwenye mikataba ila Leo wanakuja kujitamba kuwa wao Wanapamban na ufisadi
 
Nchi ilikosa uongozi bora. Uongozi wa sasa angalau una uthubutu na ujasiri. Unatekeleza ahadi kwa vitendo

Na wewe kwa akili yako kabisa unaona huu uongozi tulionao sasa ni uongozi bora?

Yaani huu uongozi unaothubutu na kujivika ujasiri wa kufanya jambo pasipo kuwa na muono sahihi ni wapi tunaelekea ndio utatuvuja hapa kweli hili giza tuliopo?

Huu uongozi wa mtu asiyekuwa na haiba ya uongozi wala kujua mipaka ya majukumu ya nafasi aliyonayo ndio uongozi bora kuliko awamu zote zilizopita?

Kwa hiyo unaamini huu uongozi ndio utatotoa kwenye utegemezi na matatizo mengine tuliyonayo!?
 
Maneno yako niliyoyawekea rangi nyekundu ni vyema ukayaongezea thamani kuwa ya ukweli mifano hai na takwimu. Kutokufanya hivyo sintokosea kukuita nyumbu wa wabadilisha gia angani, mabingwa wa utunzi wa uzushi, wanafiki na waongo.
 
Mh. Kikwete aliulizwa swali 'kwanini Tanzania ni maskini? Jibu unalo mwenyewe. Huu umaskini haujaletwa na upinzani. Sisi wananchi wakawaida tunahoji hizo sheria´mbovu waliozitunga kwanini hawakuwajibishwa kwa kulitia taifa hasara.
 
Nchi ilikosa uongozi bora. Uongozi wa sasa angalau una uthubutu na ujasiri. Unatekeleza ahadi kwa vitendo
jambo kubwa ni kuweka uwazi kwenye mikataba na kila kitu kinachofanywa na serikali, mimi na wewe na wananchi kwa ujumla sisi ndio wamiliki wa hizi rasilimali, sio raisi, sio CCM, sio Chadema wala taasisi nyengine.

Hivyo wananchi wanatakiwa wajulishwe kila kitu ikiwemo hayo makubaliano, tunaweza shangilia au kuponda then. tukaja kujuta huko baadae.
 
Maneno yako niliyoyawekea rangi nyekundu ni vyema ukayaongezea thamani kuwa ya ukweli mifano hai na takwimu. Kutokufanya hivyo sintokosea kukuita nyumbu wa wabadilisha gia angani, mabingwa wa utunzi wa uzushi, wanafiki na waongo.
Kwa hiyo unataka kusema si sahihi kwamba hii serikali ina mapungufu kwenye maamuzi yake mengi inayofanya!? Seseke la ACCACIA mmewashinikiza TRA kutoa taarifa za kodi bila kumaliza mchakato nzima na kujiridhisha kwanza kiasi sahihi cha kodi wanayodaiwa, wakatoa taarifa ambazo hazina uhalisia wowote matokeo yake sasa hivi mnalipwa 0.9% ya zile hela umlizo jipangia kulipwa awali eti trillion 400!! Sasa huo kama sio ukurupukaji na kukosa maono ni nini?

Nchi ina madeni na inazidi kukopa na bajeti inazidi kupanuliwa tu kila mwaka wakati huo biashara na vyanzo vingine vya mapato ya ndani vinazidi kufifia tu, wakina Zito wakisema tena kwa ufafanuzi wanaitwa wasaliti,wachochezi na hata kutolewa uhai.

Raisi hajui mipaka ya kazi yake, hajui sheria ya mashirika ya uma inasemaje, hajui nini maana ya soko huria!

Yaani yeye akiamka anamaua anamua waongezewe mishaara au wasiongezewe, kazi za wizara ya fedha yeye ndio mtoa oders na wala sio waziti tena, soko la ndani kwa bidhaa nyingi za mazao limekufa halafu bado anafunga mipaka kupeleka nje bidhaa.... Sasa raisi kama huyu bado unasema ana haiba ya uongozi!?
 
Serikali ya awamu ya tano ni serikali ya ovyooooo kuliko zote zilizopita.

Ni mwendowazimu pekee tu ndio atakaye amini kila inachokifanya..
 
Kwa hiyo unataka kusema si sahihi kwamba hii serikali ina mapungufu kwenye maamuzi yake mengi inayofanya!? Seseke la ACCACIA mmewashinikiza TRA kutoa taarifa za kodi bila kumaliza mchakato nzima na kujiridhisha kwanza kiasi sahihi cha kodi wanayodaiwa, wakatoa taarifa ambazo hazina uhalisia wowote matokeo yake sasa hivi mnalipwa 0.9% ya zile hela umlizo jipangia kulipwa awali eti trillion 400!! Sasa huo kama sio ukurupukaji na kukosa maono ni nini?

Nchi ina madeni na inazidi kukopa na bajeti inazidi kupanuliwa tu kila mwaka wakati huo biashara na vyanzo vingine vya mapato ya ndani vinazidi kufifia tu, wakina Zito wakisema tena kwa ufafanuzi wanaitwa wasaliti,wachochezi na hata kutolewa uhai.

Raisi hajui mipaka ya kazi yake, hajui sheria ya mashirika ya uma inasemaje, hajui nini maana ya soko huria!

Yaani yeye akiamka anamaua anamua waongezewe mishaara au wasiongezewe, kazi za wizara ya fedha yeye ndio mtoa oders na wala sio waziti tena, soko la ndani kwa bidhaa nyingi za mazao limekufa halafu bado anafunga mipaka kupeleka nje bidhaa.... Sasa raisi kama huyu bado unasema ana haiba ya uongozi!?
Jibu lako hilo linaonesha ni la kukurupuka. Soma taarifa kamili kuhusu makubaliano yaliyofikiwa.
 
Kumekuwa na maneno ya kejeli na kebehi kwa Rais Magufuli kutokana na hatua zake anazochukua kulinda na kusimamia rasimali za taifa.

Ni kweli kabisa Tanzania ni moja ya nchi duniani zilizo na utajiri usiopimika, ambao ukisimamiwa vizuri, wananchi watakuwa matajiri kuliko wale wa nchi za Kiarabu, ambao wanategemea tu mafuta.

Nitoe mifano michache tu ya utajiri wa nchi hii kwa kilimo, ufugaji, utalii, uchimbaji madini, uzalishaji wa nishati, nk:
1) Ardhi yenye rutuba kwenye mabonde ya mito mikubwa isiyopungua saba:- Pangani, Rufiji, Mara, Kagera, Ruvu, Wami, Great Ruaha, Ulanga, Ruvuma, Rufiji, Malagalasi, nk

2) Maziwa ya maji baridi:- Tanganyika, Victoria, Nyasa, Manyara, Eyasi, Rukwa, NayronJipe, Chala, Babati, Duliti-See, nk

3) Ukanda wa bahari ya Hindi wenye urefu wa 1,424km

4) Mbuga zenye wanyama wa kila aina:- Arusha, Mkomazi, Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro, Ziwa Manyara, Serengeti, Tarangire, Gombe, Katavi, Mahale, Rubondo, Saanane, Kitulo, Mikumi, Ruaha,Milima ya Udzungwa, Sadani, nk.

5) Gasi, mafuta na aina mbalimbali za madini kama vile ya
(i)viwandani, km Diamond (Almasi), Gold (Dhahabu), Copper (Shaba), Tanzanite, Ruby, Iron (Chuma), Soda ash, Salt (Chumvi), Limestone (Chokaa), Gypsum, Gravel (Changarawe), Sand (Mchanga), Graphite, nk
(ii) Nishati km , Coal (Makaa ya mawe), na Uranium.

6) Zaidi ya asilimia 10 (10%) ya eneo lenye uwezo wa kuzalisha nishati ya umeme wa jua na upepo, ukubwa ambao ni sawa na taifa la Malawi, kiwango kama cha Hispania lakini zaidi ya jimbo la California, Marekani. Kwa mfano: ukanda wa kati (Mkoa wa Dodoma na Singida); ukanda wa kasikazini mashariki (Mkoa wa Kilimanjaro)

Hivi kwa utajiri wote huo, ni halali nchi iendelee kuwa omba omba! Kama alivosema leo Rais, akiwapa vyeti wanakamati ya makinikia, Tanzania imekuwa ikitowa misaada (donate) kwa ujinga na unyonge wetu, kumbe tunaibiwa.

Lakini viongozi wa upinzani, na mbeleko zao humu jamvini wako mbele kutetea na kulinda unyonge wao kwa kuwapigia mabwana zao.

NI AIBU kwao. Ifikapo 2020, wapinzani wataweza kweli kusimama majukwaani kujibu maswali ya Watanzania, kuhusu kauli na matendo yao?

Nawasilisha.

Cc Paskali, Mzee Mwanakijiji, Jingalao
 
NI AIBU kwao. Ifikapo 2020, wapinzani wataweza kweli kusimama majukwaani kujibu maswali ya Watanzania, kuhusu kauli na matendo yao?
Tutaendela kubaki masikini milele sababu, mawazo yako na CCM kwakila wanachokifanya wanafukiria uchaguzi, hawaliweki Taifa kwanza, wao uchaguzi mkuu na kushinda kwanza.
 
Kwa kauli hiyo, upinzani unaishi katika ndoto za alinacha. Kama viongozi wa upinzani na wafuasi wao hwatakuwa na mawazo chanya kuona na kushiriki kuleta mabadiliko ya kijamii, kisias na kiuchumi, watakuja kustuka mwaka 2020 na wasiwe na la kuwaambia wapiga kura.

Iwapo viongozi wa upinzani wana nia njema na nchi yao waachane na siasa za chuki na fitina. Haziwasaidii kwa kuwa Watanzania siyo malighafi ya viwanda vyao vya chuki wanavyovijenga kwa kasi.
 
Kuwa na raslimari nyingi sio utajiri utajiri ni kufahamu matumizi ya raslimari ulizo nazo umaskini wa mawazo ni umaskini mkubwa kuliko umaskini wowote duniani kwa maana hiyo sisi ni maskini duniani kuliko nchi nyngn yeyeto
 
Back
Top Bottom