MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Wasalaa wanajamvi,
Kama ni masuala ya kina ndugu Paulo, Ubunge wa mama Salma na mengine kuendelea kuyajadili ni kupoteza muda.
Kama kuna mtu ametumia cheti cha mtu mamlaka zipo zitashughulika nalo kisheria na lazima awajibishwe, hivyo tuendelee na ajenda muhimu kwa taifa hayo mengine tuachane nayo.
First Lady mstaafu kuteuliwa kua Mbunge ni haki yake kikatiba, hakuna sehemu anazuiliwa kua mbunge na hata kugombea urais inawezekana pia kwake. Kwahiyo kutumia muda mwingi kulijadili hilo ni kupotea.
Taifa liko kwenye vita dhidi ya madawa ya kulevya, tatizo la ajira, mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, madai ya walimu,katiba mpya, ukame na upungufu wa Chakula.Hizi ndizo ajenda muhimu kujadili na kuisukuma serikali kuchukua hatua madhubuti na sio kelele zisizokua na faida kwa umma.
Nasitiza;
Kama kuna mtu anatumia vyeti vya mwenzake popote alipo, umma utajua na itashangaza asipochululiwa hatua kama wengine.Uchunguzi ufanyike dhidi yake halafu matokeo yatolewe! Ila usiwe ni kama furaha kwa sababu flani flani ispokua ichukuliwe kama bahati mbaya kwake kama ilivyo kwa wengine waliokutwa na madahibu hayo.