Nchi imeingia mdudu

malisak

Platinum Member
Joined
Mar 16, 2006
Posts
739
Reaction score
852
Naandika Uzi huu huku Nikiwa nimegubikwa na huzuni nyingi na masikitiko makubwa sana. Nchi yetu imekuwaje?

Ile nchi tulioisifu kwa mapambio, tungo na ngonjera za kuvutia kwani kuna laana ilioachwa na waasisi Baba wa taifa Mwl. Nyerere na akina Mkwawa? toka kipindi cha kupata Uhuru na Hatujui? Hatusikilizani tena, hatuelewani tena na hatuheshimiani tena.

Ni masikitiko makubwa Sana kuona mkanganyiko juu ya kishika madaraka, demokrasia umekufa, Uhuru imetoweka, tumedhuriwa na hofu na taharuki kila Wakati. Kwani tumekosea wapi? Kila nikitafakari nakosa majibu.

Kuna Muda nakumbuka maneno ya waziri ya fenda "Hamieni Burundi" kila nikitafakari Ile kauli ni kama ilikuwa na unabii uliojificha ambao muheshimiwa aliuchukulia kama mzaha Lakini kuna kaukweli ndani Yake.

Sitaki kusikia wala sitamani na Sisi siku moja tuwe wakimbizi, natamani Amani yetu,umoja na mshikamano wetu na kama kutawala na hofu basi iwe na hofu ya Mungu Tu. Nikitazama video za wenzetu waliopoteza Uhuru na Amani yao napata hisia mbaya juu ya hatma ya kizazi chetu kama itatokea tukakiacha huko siku zijazo.

Jasho la maumivu na hofu linanimwagika,machozi ya damu yanavuja moyoni mwangu nikitafakari Nyakati. Natamani Muda urudi Nyuma,natamani ule upendo wetu uliotukuka mpaka kubatizwa jina la kisiwa cha Amani. Hebu tushushe silaha chini na tusalimu amri kwa manufaa ya nchi yetu.

Natamani kuona tukicheka na kutabasamu pamoja tena mbele ya majukwaa yenye kumiliki midahalo ya mgongano wa mawazo yenye kujadili mustakabali wa nchi yetu hii Nzuri ya kuvutia.

Mungu bariki na uwezeshe Amani ya nchi hii irejee na kudumu kama zamani. Naamini hakuna kinachoshindikana chini ya jua tukikubali kujishusha. Mungu tusaidie.
 
Shida sio kwamba kuna kitu kimebadilika.
Nchi ni Ile Ile
Watu ni walewale
Ccm ni ileile
Katiba na tume ya uchaguzi ni ileile
Viongozi wa dini ni walewale
Bunge ni lilelile
Mahakama ni zilezile
Lugha ni ileile.

Kwanza hatukuwahi kuwa na amani ila tulikuwa na ujinga ambao tuliuita amani.
Hatukuhoji,
Hatukuuliza,
Hatukusema,
Hatukulalamika,
Hatukufurahi ,
Hatukulia ,
Hatuomboleza.

Ni kama tulikuwa hatujui Nini kinatokea na kipi kitatokea.kila mtu kwasababu ya ujinga tunaouita amani tuliamua kukaa kimya na kujifanya hayatuhusu japo yalituumiza.

Kwani tumebadilika?Jibu ni hapana ila tu kuna baadhi ya watu wameanza kuchoka kuvumilia kuishi ndani ya ujinga unaoitwa amani.

Mtaji wa kinachoitwa amani ya nchi hii ni "ujinga".kadri jamii inavyopiga hatua za taratibu kupunguza kiwango Cha ujinga ndivyo amani yetu inavyozidi kuwa shakani.

Tujitahidi saana kuimarisha kiwango Cha ujinga katika jamii yetu na amani itazidi kutamalaki
 
Ni kweli kabisa Lakini hakuna hatari zaidi kama kujua Aina ya Simu inayokuua na huwezi kujinusuru ni heri ubaki kizani. Sababu Huo ukweli mchango tulishajengewa hofu iliogeuka mazowea sasa basi tunafurukuta huku tunamalizwa kimya kimya. Ukweli unajulikana ila ukijaribu kujitetea ni makosa sasa tusimame upande gani sasa
 
Mama atajua mwenyewe No Reforms No Election
 
Nani ajishushe go straight
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…