Nchi iko Pabaya Sana: Watanzania tufanye nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi iko Pabaya Sana: Watanzania tufanye nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nyami2010, Feb 3, 2012.

 1. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wana Jamii

  Nionavyo mimi, hali ya NCHI ni TETE kuliko tulivyozoea. Baadhi ya viashiria ni hivi hapa:

  1. Hazina ni kweupe. Mhe. Waziri Mkuchika alibainisha hili, japo Serikali imekuwa ikipinga muda mrefu. Ona sasa Mhe. Rais analazimika kupunguza baadhi ya maafisa wake kwenye safari za nje
  2. Bunge kwa namna moja au nyingine halina imani na Rais. Mhe. Spika alisema Rais amebariki posho za Waheshimiwa Wabunge, Ikulu ikakana. Kumbuka sakata la Jairo na Luhanjo
  3. Viongozi wetu wameanza kupeana sumu....hadi wanaogopa kupeana mikono. Sakata la Mhe. Mwakyembe
  4. Ndani ya vyama hakupikiki. Magamba ya CCM, Mhe. Kafulila, Mhe. Hamad.....
  5. Uchumi umekufa:
  -Mfumko wa bei ni takribani 20% leo....ukitoka 4% mwaka 2005.
  -Serikali imeshindwa kutoa fedha za maendeleo kwenye halmashauri zote nchini, Waziri wa TAMISEMI amekiri hayo Bungeni jana.
  -Serikali imeshindwa kununua vifaa vya tiba na kutoa viposho vidogo vidogo kwa madaktari
  6. Hali ya Maisha miongoni mwa Watanzania tulio wengi ni mbaya sana X sana!
  7. Serikali kupitia Waziri Mkuu imekubali kuwa imeshindwa kuwaletea wananchi maisha bora. Tazama gazeti la Tanzania Daima la leo tar 3 Feb 2012.
  8. Viongozi wa Serikali wakiwemo Wabunge wanajitazama wao tu...., wanaacha raia tunakufa..........
  9.....ongeza list

  Hivi katika hali kama hii, watanzania twaweza kufanya nini? Ebu tupeane mawazo na mikakati kisha tuamue, la sivyo tunazidi kuangamia!
   
 2. S

  Shansila Senior Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa nchi nyingine,kingeshanuka,ila kwa sababu ni Tza watu watakwambia ooh amani hii ni lulu,wakati hayo yote uliyosema ndio viashiria vya kutokuwa na amani.
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkuu!

  Hakika hali ni tata mbaya kbs na Mi ninachoona cha kufanya ni Nguvu ya Umma inyanyuke tu kuinusuru Taifa letu ambalo hakuna raslmali ambayo hakuna.

  Hasa uongozi wa ngazi ya juu ktk serikali tawala wote wangetakiwa wapanguliwe,Hawana faida kwa Watanzania wanatikiswa na uchumi duni iliyosababishwa na watu wachache kwa ajili ya matumbo yao.
  Hili linaniuma sana!
   
 4. s

  sawabho JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Yote haya ni kwa ajili ya kupima uvumilivu na uaminifu wenu. Maana hali hii itakuja kuwa rejea katika miaka ijayo.........kama tuliweza kuvumilia mwaka 2011/12 .........
   
 5. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hatuna cha kufanya, kwasababu tulishaamua kwamba kikwete hatufai na hatukumchagua lakini Tume ya Taifa ya uchaguzi ikatangaza kwamba ameshinda na ikatokea jimbo la Nyang'wale na Geita matokeo yanafanana kila kitu. Nadhani tumuachie Mungu au tumuweke mungu pembeni tuwatoe kwa nguvu wanao roga nchi yetu
   
Loading...