Nchi haiwi ya kisheria ikiwa kiongozi hawezi kushtakiwa

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Written by santorini // 18/03/2012 // Habari // 4 Comments


Nchi yoyote duniani ikipitisha sheria ya kusema Raisi asishtakiwe ni nchi yenye ubaguzi wa hali ya juu.
Hizi ni fikra zangu ,sasa ikiwa yeyote ambaye anapingana na fikra zangu anayo haki ya kupingana nazo kwani fikra za binaadamu wote zinatofautiana ,ila uwanja huu wa mzalendo upo wazi kutoa fikra zake mtu binafsi kwa faida ya umma na umma ukaangalia na kupima nani sahihi katika kupingana huko.

Mawazo yangu sikusudii kuibana nchi fulani au jamii fulani lakini nakusudia kama nilivyotangulia kusema nchi yoyote duniani.
Ni kwa nini ikiwa wewe ni kiongozi wa nchi na unahubiri utawala wa sheria kwa wote na huku unajiwekea kutokushtakiwa ? kwani unaogopa nini.kwa nini hujitangazii ufalme ikawa ndio mmiliki wa kila kitu na uwe above the law.

Fanya utakalo mbele ya binaadamu wenzio maadam mkono wako mrefu jiwekee vizingiti uvipendavyo vya kutokushtakiwa lakini mwisho wa hesabu ni ziro utafika katika mahakama ya muadilifu.

Hesabu zote duniani ni kumi yaani moja mpaka tisa na ya kumi ni zero andika mabilioni ya nambari na hesabu lakini utakuwa ukirudia rudia nambari zile zile tisa na ziro.

Ukijiamulia kwamba mimi nisishtakiwe umeshajiweka katika hali ambayo ni tofauti na wote unaowaongoza yaani wewe si katika wao,labda astaghfirullah,hainifalii mimi tutamka hapo kwani nataraji imeshafahamika madda yangu hapa.

Hata baba wa nyumba anapofanya utumbo kwa watoto wake aliyowazaa watoto humshitaki baba yao kwa mama yao kwani huwa ndio njia pekee wanayoiweza kuitumia ,lakini ikiwa watoto wenyewe ni baleghe zaidi huweza kumshtaki baba yao katika mahkama ua sehemu yoyote ya kisheria japo kwa sheha.

Namalizia kwa kusema hapana utawala wa sheria ikiwa mmoja wetu akifanya kosa asishtakiwe.
 
anaweza kushtakiwa ila inabidi awe 'impeached' kwanza kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na katiba.

Written
by santorini //
18/03/2012 //
Habari //
4
Comments

Nchi yoyote duniani ikipitisha sheria ya kusema Raisi asishtakiwe ni
nchi yenye ubaguzi wa hali ya juu.
Hizi ni fikra zangu ,sasa ikiwa yeyote ambaye anapingana na fikra zangu
anayo haki ya kupingana nazo kwani fikra za binaadamu wote
zinatofautiana ,ila uwanja huu wa mzalendo upo wazi kutoa fikra zake
mtu binafsi kwa faida ya umma na umma ukaangalia na kupima nani sahihi
katika kupingana huko.
Mawazo yangu sikusudii kuibana nchi fulani au jamii fulani lakini
nakusudia kama nilivyotangulia kusema nchi yoyote duniani.
Ni kwa nini ikiwa wewe ni kiongozi wa nchi na unahubiri utawala wa
sheria kwa wote na huku unajiwekea kutokushtakiwa ? kwani unaogopa
nini.kwa nini hujitangazii ufalme ikawa ndio mmiliki wa kila kitu na
uwe above the law.
Fanya utakalo mbele ya binaadamu wenzio maadam mkono wako mrefu jiwekee
vizingiti uvipendavyo vya kutokushtakiwa lakini mwisho wa hesabu ni
ziro utafika katika mahakama ya muadilifu.
Hesabu zote duniani ni kumi yaani moja mpaka tisa na ya kumi ni zero
andika mabilioni ya nambari na hesabu lakini utakuwa ukirudia rudia
nambari zile zile tisa na ziro.
Ukijiamulia kwamba mimi nisishtakiwe umeshajiweka katika hali ambayo ni
tofauti na wote unaowaongoza yaani wewe si katika wao,labda
astaghfirullah,hainifalii mimi tutamka hapo kwani nataraji
imeshafahamika madda yangu hapa.
Hata baba wa nyumba anapofanya utumbo kwa watoto wake aliyowazaa watoto
humshitaki baba yao kwa mama yao kwani huwa ndio njia pekee wanayoiweza
kuitumia ,lakini ikiwa watoto wenyewe ni baleghe zaidi huweza kumshtaki
baba yao katika mahkama ua sehemu yoyote ya kisheria japo kwa sheha.
Namalizia kwa kusema hapana utawala wa sheria ikiwa mmoja wetu akifanya
kosa asishtakiwe.
 
Back
Top Bottom