Kwangu mimi nchi inajengwa na mtu mmoja,ambaye ni kiongozi wa nchi.Yeye akisimamia anacho amini na kukitekeleza kwa asilimia kubwa basi nchi itasonga mbele.Mifano ipo mingi ingawa sio mingine mizuri lakini ile dhana ya kiongozi kuindeleza nchi yake ipo.Mfano hai ni Hitler wa Ujerumani.Yeye dhamira yake ilikuwa kuitawala dunia,hivyo akaelekeza nguvu zake katika jeshi bora la kupigana vita.Mfano wa pili ni George Washington ,yeye aliamini katika umoja wa taifa la Marekani,alijieleza katika hilo na kufanikiwa kuunganisha zaidi ya nchi 50 kuwa moja.Yupo Mao ailyeamini katika Ukomonist wa utajiri amejieleza katika hilo na leo hii China inatisha kiuchumi.Hata hapa kwetu mwalimum alitutoa katika ubepari wa kurithi kwa Waingereza kutuleta kewnye ujamaa.Ni dhamira ya aliye juu, inasababisha ama nchi iendelee au irudi nyuma,muongozo wake ndiyo dira ya nchi.