NCCR-Mageuzi kuboresha miundo mbinu mshuleni

NCCR Mageuzi

Member
Oct 3, 2007
23
63
Chama cha NCCR-Mageuzi kimeendelea na ziara zake za kampeni kwenye mikoa mbalimbali nchini Tanzania, lengo likiwa ni kuomba kura kwa wananchi ili kuweza kuunda serikali kwa ajili ya kuwatumikia wananchi katika kipindi cha miaka 5 ijayo.

Akiwa Wilayani Chemba Mkoani Dodoma, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha NCCR-Mageuzi ndugu Yeremia Kulwa Maganja katika baadhi ya mambo ambayo ameyasemea ni pamoja na uboreshaji wa miundo mbinu ya shule hasa ujenzi wa vyoo bora pamoja na miundo mbinu wezeshi kwa watoto wa kike ili kwa ajili ya mahitaji yao.

"NCCR-Mageuzi tutabadili miundo mbinu ya shule zote na kuwa na madarasa na vyoo bora na vya uhakika ili kuhakikisha wafunzi wa jinsia zote wanakuwa na sehemu maalum kwa ajili ya mahitaji yao.

3 (2).png
 
KWA ATAKAYE IBA KURA BORA APATE UGONJWA WA UKICHAA MILELE MAANA WATU HAWA WANATUZUNGUSHA VICHWA SANA TUTAOMBA MASAADA SOUTH KOREA (WOTE HATUWEZI KUWA WATOTO)
 
Back
Top Bottom