NCCR kushirikiana na Chadema bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NCCR kushirikiana na Chadema bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 27, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma

  CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimekubali kufanya kazi bungeni na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Taarifa zilizopatikana jana mjini hapa zinasema baada ya hivi karibuni vyama vya upinzani nyenye wabunge kuanza mazungumzo ya kushirikiana, wabunge wanne wa NCCR-Mageuzi wameridhia hatua hiyo kwa kuwa wanaamini umoja wao unaweza kuzaa matunda bungeni.

  Kutokana na hali hiyo, taarifa hizo zinasema wabunge hao wanne tayari wamemwandikia barua Katibu Mkuu wa chama chao, Samwel Ruhuza kumjulisha nia yao hiyo licha ya awali kuwapo kwa kutofauti za kisiasa baina ya chama chao na CHADEMA.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, Ruhuza anatarajia kuwajibu wabunge hao wakati wowote wiki hii mchakato wa ushirikiano uweze kukamilika baada ya kikao cha mwisho cha vyama hivyo kufanyika.

  Hata hivyo, Ruhuza alipozungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu jana akiwa Kigoma alikataa kueleza kwa undani mazungumzo ya vyama hivyo kwa kile alichosema kuwa anaweza kutafsiriwa vibaya na wanasiasa wenzake juu ya ushirika huo.

  "Suala la ushirikiano wetu naomba nisilizungumze kwa sasa kwa sababu naweza nikalizungumza kisha nikatafasiriwa vibaya na watakaosoma taarifa hiyo.

  "Kama mazungumzo yapo, mtaelezwa na kama hayapo pia mtaelezwa kama tutaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo. Hili suala la wabunge kuniandikia barua pia liache kama lilivyo, sipendi kulizungumzia, siwezi kusema nimeshaipata hiyo barua au bado, naomba uliache.

  "Lakini, jambo la msingi hapa ni kwamba, sisi kama NCCR-Mageuzi tunaamini katika ‘alliance' (ushirikiano)… tunaamini tukifanya kazi kwa kushirikiana na wenzetu tufafanikiwa zaidi kwa kuiwajibisha serikali na hatimaye kushika dola," alisema Ruhuza.

  Naye Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) alikiri kuwapo kwa mazungumzo kati ya vyama vya upinzani vyenye wabunge.

  "Mazungumzo yapo na yanaendelea vizuri, sisi wabunge wa NCCR-Mageuzi tuko tayari kushirikiana na wenzetu kwa sababu tunaamini ushirika ni muhimu katika kujiimarisha kisiasa na hata wananchi wenyewe wanaamini wapinzani tukishirikiana tutafanya kazi kwa mafanikio zaidi.

  "Unaweza ukajiuliza kwa nini tunakubali kushirikiana na CHADEMA wakati tulikuwa na uhasama, jibu ni kwamba tofauti hazina umuhimu katika kuleta maendeleo na ndiyo maana unaona sasa CCM na CUF wameunda Serikali ya mseto kwa masilahi ya Wazanzibari.

  "Hata wapalestina na waisrael wanakaa na kuzngumza kila wakati licha ya tofauti zao, kwa hiyo sisi hatuoni tatizo maana matatizo siku zote yanazungumzika na ili muishi kwa amani lazima mkae, mzungumze.

  "Kwa kutambua hilo, tayari tumeshamwandikia barua katibu mkuu wetu mkuu kumjulisha azma yetu, kwa hiyo, mambo mengine unaweza kumuuliza katibu wetu. Mimi siwezi kuzungumza zaidi," alisema Kafulila.

  Chanzo chetu cha habari kilichoko mjini hapa kilisema kuwa wabunge hao wa vyama vya upinzani wamekwisha kukaa vikao viwili ambavyo viliongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe katika ofisi yake ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni.

  Taarifa hizo zinasema katika kikao cha kwanza, TLP iliwakilishwa na Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema, NCCR-Mageuzi iliwakilishwa na Kafulila, CUF iliwakilishwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya na Mbunge wa Bariadi Magharibi Mashariki, John Cheyo hakuhudhuria.

  Pamoja na vikao hivyo kufanyika kwa nia nzuri, taarifa zinasema kuwa wawakilishi wa TLP na CUF waliwashambulia Chadema kwa kile walichosema kuwa chama hicho kimekuwa kikiwashutumu kuwa TLP na CUF ni CCM B.

  Hata hivyo, baada ya majadiliano ya kina, wanasiasa hao walishusha hasira ingawa hawakusema kama wako tayari kuunda kambi ya upinzani isipokuwa NCCR-Mageuzi ambao wameshakubali kuunda kambi moja ya upinzani na Chadema.

  Februari mwaka huu, Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alitangaza bungeni baraza lake la mawaziri ambalo liliundwa na wabunge wa CHADEMA pekee.

  Hatua hiyo ilizua mjadala kwa baadhi ya wanasiasa wengine wakisema kuwa kitendo cha vyama vingine kutoshirikishwa katika baraza hilo kinadhoofisha nguvu ya upinzani ambayo inatakiwa kwa ajili ya kuiwajibisha Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
   
 2. F

  FUSO JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,297
  Trophy Points: 280
  mimi sina tatizo kwa hili - ila huyu jamaa ( Mbatia) afute kesi ya kawe fasta.
   
Loading...