NBC YATAKA VIKUNDI IKOPESHE WAKULIMA, WAFUGAJI

NBC YATAKA VIKUNDI IKOPESHE WAKULIMA, WAFUGAJI

neema shamuhenya

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
312
Reaction score
216
BENKI ya NBC inatarajia kutoa mikopo kwa wakulima, wavuvi na wafugaji ikiwa ni hatua ya kuwekeza katika maendeleo ya wananchi.

Akizungumza na waandishi kwenye banda la benki hiyo katika maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki mkoani Simiyu, Mkuu wa Uhai wa Wateja NBC, Gaudence Shawa alisema mpango huo uko mbioni kutekelezwa.

Ili kuwa na uhakika wa kunufaika na mikopo hiyo, makundi hayo walengwa yametakiwa kujiunga katika vikundi vya uzalishaji irahisishie benki kuwafikia na kuwatambua.

"Tunatoa mwito kwa wakulima, wavuvi na wafugaji kujiunga katika vikundi na sisi tutatoa mikopo kupitia wadau mbalimbali kama vile Baraza la Uwezeshaji (NEEC)," alisema Shawa.

Alisema maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi, yamewawezesha kukukutana na makundi hayo na kuwaelimisha umuhmu wa kukopa na kuendesha kilimo chenye tija.

“Tumekutana na wakulima, wafugaji, wavuvi na wadau wengine...NBC tunajivunia , tumepata mafanikio katika ukuzaji kilimo, uvuvi na ufugaji,"alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini ameiomba benki hiyo ya NBC kufikisha huduma zake mkoani humu ili kupanua wigo wa huduma za kibenki.

Sagini alisema mkoa wa Simiyu una matajiri wengi wakiwemo wafugaji na wakulima ambao wanahitaji kupatiwa huduma za kibenki waepuke kuhifadhi fedha nyumbani.

Alitoa mfano wa mnada wa kila wiki katika eneo la Dutwa na kusema wafanyabiashara husika warahisishiwe kwa kuletewa huduma nyingi za kibenki.

Meneja Mahusiano wa NBC, William Kalaghe alisema hivi karibuni watakuwa mkoani humo kwa huduma za kudumu.

Alisema katika hatua ya kwanza, wiki ijayo watazindua wakala mkuu wa benki atakayetoa huduma mjini Bariadi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom