Nbc bank kuna mgomo baridi?

POMPO

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
6,690
2,400
Wadau! Habari zimezagaa mjini kuwa, Kuna dalili zote za kutokea mgomo mkubwa ndani ya NBC Bank, ile bank iliobinafsishwa kwa makaburu kwa bei ya chee, sasa kuna mgomo baridi, wafanyakaz wananyanywaswa sana, wameongezewa muda wa kutoka oficn kinyume cha sheria za kazi, pia mishahara na bonus kiduchu, huku menegment ikila bata, zaidi ya million150, kwa mtu mmoja wakati teller laki3.

My take: kama ni kweli ngomeni fasta, mpaka kieleweke: tupo nyuma yenu.
Wakuu hii imekaa vp?
 
Hii benki imeporoka sana kiutendaji mwaka 2010. Kwa hali ya kawaida kama wewe ni mmowapo ya wamiliki lazima utegemee kuona utawala unachukua hatua mahsusi. Kwanza, kujinasua kutoka hapo walipo. Pili, kuongeza uzalishaji ili kupata faida kubwa ya kuwawezesha kutoa gawio zuri na kuongeza thamani ya hisa.

Sasa kwa hali kama walionayo NBC hivi sasa suala la kupunguza gharama za uendeshaji linakuwa linatangulizwa sana kama hakuna njia mbadala. Hii ikitokea wafanyakazi ndio wa kwanza kuathirika kwani marupurupu yanayoendana na kazi hupunguzwa au kusitishwa kabisa. Sasa kama kuna upendeleo na hakuna ushirikishwaji basi watawala wategemee kupambana na matatizo. Hizo ni harakati za wafanyakazi kujaribu kunusuru hali zao za maisha.
 
Back
Top Bottom