Nbc acheni usanii huu

Nbc acheni usanii huu

structuralist

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,230
Reaction score
909
Kama tunavofahamu jumamosi benk nyingi hufungwa sa sita mchana. Sasa katika mishemishe nikalazimika kulipa mahali kama 1.3 milioni,hivo nikaona ngoja nikachomoe fasta kwenye ATM za NBC( MOSHI) . Kilichotokea ni kwamba kila ATM inasema kiwango cha juu kabisa kutoa ni laki mbli(200000), (kuna ATM 4,moja ilikuwa off,yapili haikuwa na fedha,mbili zilizobakia ndio zinatoa hicho kiwango)kwahiyo nikalazimika kutoa mara sita ili angalau nipate 1.2mln. Hii si mara yakwanza kushuhudia hili,na binafsi naamini wanafanya makusudi ili kujiongezea pesa zitokanazo na makato ya kila muaamala unaofanyika. Inafahamika kuwa kiwango cha juu kilikuwa laki nne(400000)je kimeshushwa au ni wizi wa mchana kweupeeeeee.....
 
inawezekana ATM zilibaki na noti za elfu tano tano tu. machine zimewezeshwa kutoa noti 40 tu kwa muamala 1. pole sana mkuu. hope hujakosa mke:angry:
 
NMB wamebadilika! Kufungua akaunti hakuna kwenda tena kwa balozi.............. karibu huku
 
Hata mimi huwa inanitotokea tena sana sana ile atm ya kariakoo sokoni.
Ni wizi tu!
Kama no hivyo kwani nini wasiweke noti za sh. Elfu kumi kumi.
BOT mko wapi?
 
yaap zilitoka hizo za buku tanotano,so kumbe hiyo ndio sababu,ila kwanini zote waziweke hizo buku tano tano ilihali wanajua kunawatu watatoa kama m hvi

Mimi si mtu wa benki, ila nadhani inategemea na upatikanaji wa noti, ila hilo haliathiri kwa vyovyote kiwango unachotoa, kama max ni 1.2 basi na utaitoa kama kawaida. Na buku tanotano haziwezi zikatoka kwa laki 4 in a go maana ni rundo kubwa. Uwe na amani mkuu, imeshanitokea Stanbic na nikapata majibu baada ya kuuliza kulikoni.
 
Wakuu poleni. ATM za NBC huwekwa noti za 10,000 na 5,000 kwa uwiano wa 6:2 au 3:1 sawia. Hivyo kiwango cha noti za 10,000 huwa ni kikubwa sana. Ni kwa vile noti za 10,000 huisha kwanza ndo zile za 5000 humalizia. Poleni kwa wote mliopata kusumbuka.
NB: KIWANGO CHA JUU KUTOA HELA NBC NI SH. 1,500,000 KWENYE
ATM KWA SIKU.KUHAMISHA FEDHA KWENDA AKAUNTI NYINGINE KWA NBC MOBILE
NI SH.MILIONI KUMI KWA SIKU, KWENDA M PESA NI 1,500,000 KWA
SIKU.🙂:smile-big:
 
Pole Sana ndugu hao makaburu wamekuja kutunyonya mm ni mteja wa Exim bank ila nimekuwa nikitumia ATM ya nbc oil com hapa science DSM kwa Kuwa zote ni VISA nimekwenda kuchek bank statement yangu nimekuta nimekatwa tzs 6000 kwa kila muala badala ya 1500 Wizi mtupu nimeapa kutotumia ATM za Hawa makaburu in my life.
 
Wakuu poleni. ATM za NBC huwekwa noti za 10,000 na 5,000 kwa uwiano wa 6:2 au 3:1 sawia. Hivyo kiwango cha noti za 10,000 huwa ni kikubwa sana. Ni kwa vile noti za 10,000 huisha kwanza ndo zile za 5000 humalizia. Poleni kwa wote mliopata kusumbuka.
NB: KIWANGO CHA JUU KUTOA HELA NBC NI SH. 1,500,000 KWENYE
ATM KWA SIKU.KUHAMISHA FEDHA KWENDA AKAUNTI NYINGINE KWA NBC MOBILE
NI SH.MILIONI KUMI KWA SIKU, KWENDA M PESA NI 1,500,000 KWA
SIKU.🙂:smile-big:

nbc mobile unajiungaje sijawah isikia hii.
 
nenda kwenye tawi lolote la nbc lililo karibu nawe. Kuna form utajaza na watakuunganisha.

Mi nilishawahi kwenda kwenye tawi lililo karibu nami,nkaambiwa niende kwenye tawi nilofungulia akaunti,sikwenda kwa kuwa lipo kushoto nami kwa mda huu.Heri mwelekeze aende alipofungulia akaunti yake.
 
Ondoa shaka karibu tena NBC kwasasa NBC Mobile tunakuhudumia popote fasta.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom