Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Rapa Nay wa Mitego amefunguka na kuweka wazi kuwa katika wanamuziki wakubwa Tanzania na wazuri kimuziki kwake Ali Kiba ni namba moja na akamtofautisha na Diamond ambaye amemtaja kuwa ni msanii mzuri kibiashara lakini hamfikii Ali Kiba kwa ubora wa kufanya muziki.
Nay ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Sijiwezi', amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EATV na kusema siku zote yeye amekuwa akimkubali sana Alikiba ingawa anatambua wazi mtaani kuna tetesi kuwa hawezi kufanya naye kazi kutokana na yeye kuwa na uswahiba na Diamond Platnumz.
"Watu wanajenga picha kuwa mimi na Alikiba siwezi kufanya naye kazi sababu tu ya uswahiba wangu na Diamond.
Ni kweli Alikiba sio mshikaji wangu lakini leo hii ukiuliza nikutajie wanamuziki watatu wazuri Tanzania wa kwanza nitamtaja Alikiba, lakini pia ukisema nitaje wasanii watatu wakubwa wafanyabiashara basi nitamtaja Diamond Platnumz" alisema Nay wa Mitego.