Behind the camera
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 315
- 757
Narudia tena kusema ‘MFICHA MARADHI, KIFO HUMUUMBUA’
Habari za muda huu ndugu zangu, waungwana wenzangu. BIla shaka afya zenu ni njema na mnaendelea vema kabisa na majukumu ya kulijenga taifa letu la Tanzania.
HONGERENI SANA
AMA BAADA YA UTANGULIZI
Lengo la kuandika uzi huu wa heshima, napenda kuelezea dukuduku langu kwa umma huenda siku moja uzi huu ukasomwa na ambaye anaweza kulitatua tatizo langu na kupata ufumbuzi.
Nafikiri utakubaliana na mimi kuwa kila mtu katka Maisha yake huwa ana ndoto na kutamani awe mtu Fulani ama kufanya kazi Fulani, lakini mara nyingi ndoto hizo huishia kuwa ndoto tu na si halisi.
Natumia fursa hii nami kuelezea ndoto zangu ambazo nilikuwa, ninazo na nitakuwa nazo mpaka mwisho wa umri wangu.
Mimi nilitamani sana kufanya kazi katika idara ya USALAMA WA TAIFA
Ndio namaanisha usalama wa Taifa langu la Tanzania katika sekta yoyote ambayo wao watanipangia. Uzalendo ndicho hasa kilinifanya nipende kuwa katika kulitumikia na kulilinda Taifa langu kikamilifu.
Sikufanya jitihada zozote kwani sijui wapi naweza kupata suluhisho la hitaji langu, wala sikuwa / sina mtu ambaye ana uwezo wa kunifanikishia suala langu hili pendwa.
Leo nimeona niliweke wazi katika mtandao huu nambari moja hapa Tanzani najua baadhi ya wadau watakuwemo humu. Huenda wakanisaidia.
Najua baadhi yao watanibeza na kuongea maneno yasio na nidhamu, lakini hili kwangu nachukulia kama changamoto nyingine tu za kimaisha.
Naipenda TANZANIA, Nawapenda Watanzania,
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Natanguliza shukrani zangu za dhati.
Kwa maswali Zaidi unaweza kuja PM

- Waswahili walisema “Mficha maradhi, mauti humuumbua”