Nawezaje kuwa Super dealer?

Habari wandugu...

Vigezo vya kuwa super dealer wa gas za kupikia ni zipi ...na mwenye abc ya hii biashara. Na je mtaj wa 50 ml unaweza tosha? Na changamoto zake?

Natanguliza shukran
Superdealer WA ges NI kuwa na mkataba na kampun ya gesi kwa ajili ya kusambaza gesi kwa eneo Fulani mfano wilaya Au mkoa , au kanda , Kazi yako kubwa NI kuuza ges kwa jumla na rejareja kwa mawakala na kwa wateja WA Mwisho , mawakala unawauzia kwa jumla , na wateja WA Mwisho unawauzia kwa rejareja ,
Pia Kazi yako kubwa NI kuongeza mawakala na kusimamia bei ya bidhaa sokoni katika eneo lako ,

Kampun inakuletea mzigo ambao unaununua kwa bei mnayokubaliana na wewe utauza kwa bei ya jumla kwa mawakala , hiyo bei ya kuuza kwa jumla na rejareja inapangwa na kampun sio wewe.

Million 30 inatosha Sana kuwa superdealer changamoto NI kupata hili dili , unaomba kwa kampuni husika kama utaona kuna eneo lipo na halina superdealer au waliopo ni wachache hawatoshi kuhudumia eneo hili , mfano Dar es salaam superdealers NI wengi Ila ukija mkoani kwa kila wilaya kuna superdealer mmoja Tu , kampuni pia itaangalia maombi yako pamoja na eneo

Vigezo vya harakaharaka NI lazima uwe na lesen kutoka EWURA
uwe na gari ya Tan 3.5+ kwa ajili ya kubebea ges kutoka Depo kupeleka kwenye Duka lako ,pia uwe na guta kwa ajili ya kusambaza ges mawakala wako
Hairuhusiwi kujihusisha na kampuni nyingine ya gesi , yani kama wewe NI superdealer WA Oryx hutakiwi kuwa na biashara na kampun nyingine ya ges.

Kuhusu Faida sina uhakika Sana ila naambiwa mtungi mdogo ukiuza jumlq Faida ni 1000 na mtungi mkubwa ukiuza jumla Faida ni 1,500, fikiria unahudumia wilaya kwa siku mawakala wako wakanunua mitungi midogo 200 inamaana unaprofit ya 200k per day
NI biashara ya uhakika Sana hasa ukipata kampun ambayo tayar inawatumiaji kwenye hilo Eneo , wapo wanaohonga Hadi M5 ili kupata Hii chance ,
 
Back
Top Bottom