Nawezaje kujitoa kwenye penzi ambalo limeshakufa na kumsahau huyu nimpendaye?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Ndugu zangu wana JF ninahitaji Msaada kwenu ninashindwa nianzie wapi lakini nataka kujitoa kwenye mahusiano ambayo penzi lake limefikia Kokomo kwani mpenzi wangu nimpendaye

1. Ameshapoteza interest na Mimi Licha ya mimi bado nampenda

2. Hatua tuliofikia mimi na mpenzi wangu nimeshaona hawezi kubadilika tena kwani vitu anavyonifanyia hivi sasa vinaonesha Hana love tena na mimi

3. Kwa sasa nimekuwa nikipitia maumivu makali sana moyoni nashindwa kufanya kazi zangu visa ninavyofanyiwa imefika hatua naona ni bora yaishe kila mtu aendelee na maisha ila moyoni bado nashindwa nianzaje kwani

Nataka nimtoe kabisa moyoni wangu asiwepo, pia nataka huyu mtu nimesahau kabisa, ule moyo wa kumpapatikia usiwepo tena, hata nisipowasiliana wala kuongea nae moyo wangu uwe na Amani

Nafanya haya yote baada kuona sasa penzi la mwenzangu Kwangu limeshakufa Hana tena hisia wala love na mimi
 
Tafuta kipozeo pembeni utamsahau tu!
You don't have to talk ati unamuacha wala nini just ondoka kimyakimya!.. binadamu tuna ufahamu na uelewa ataelewa tu kwamba unamaanisha nini!!.. jitahidi kuishi maisha yako humu duniani hatukuja kupeana karaha bali raha.. so ukiona kuna mtu anakuletea ugumu maisha my friend be simple muepuke tu kwani shingapi bhana..?
Hizo hisia ukijikeep busy na mambo yako zitayeyuka hakikisha unakuwa tu na kampani nzuri itakayokuweka busy.
 
Sjui utakuja kunifungulia uzi na mimi😂
Kuna vitu siwezi vifanya mama.. naheshimu private kitu kikitokea sirini usitegemee kukiona wazi!
Ukiniacha nakufa nalo moyoni simtangazii mtu!.. ila nami ukiniacha usifikirie utaniacha tu lzm kuna kitu nikupandikizie moyoni kikisumbue haiwezekani nisumbuke pekee..😂😜
 
Ushauli wangu kwakooo jinsi ya kuanza fanya yafuatayo utashinda

Kubali kutoka moyoni huyu mtu sio wangu tena kuanzia sasa

Kama hakuna kosa ulilomkosea basi mwachie tuu mungu na usijilaumu kwa haya yanayotokea

Acha kumfatilia maisha yake wala usijiangaishe kutaka kufahamu anaendeleaje

Usipende kumzungumzia mabaya yake kwa watu waliokuwa wanaufahamu uhusiano wetu na pia usiwaeleze chochote kuhusu kinachoendelea baina yenu

Ukikubaliana na haya anza kupunguza mawasiliano taratibu sana kama ulikuwa unamtafuta kwa siku mara tatu basi iwee mara moja

Ukifanikiwa katika hili utakuwa umeshavuka stage one baada ya mwezi jiandae stage two
 
ukishaamini hakua mtu sahh ndo maana kaondoka itakua rahisi sana kumsahau bt kama utakua unamuwazia kama mpenz wako haya maumivu yatakuganda mda mrefu.
 
Hili swala linahitaji akiri sana na sio kukurupuka kuchukua maamuzi ila njia pekee ya kudeal na hili jambo mimi huwa nawashauli yafuatayo fanya ivi

Hatua ya kwanza mfanye mpenzi wangu kuwa rafiki yako hivyo upunguze sana kuonyesha hisia zako kwake.

Hatua ya pili badili mtizamo wako wa maisha focus kwenye vya kimaendeleo kipindi hiki

Hatua ya tatu punguza mawasiliano taratibu kwa week angalau muwasiliane mara tatu au mbili

Hatua ya nne jifunze kukaa kimya ukiona unafanyiwa vitu ambavyo vinaumiza moyo wako hata kama unaumia kausha usichukue hatua yeyote ile kwani mwenzio anatafuta namna jinsi gani mtaachana hivyo ukiona anafanya vitu ambavyo havipendezi wee mwachee tuu

Hatua ya tano anza kumchukia mpenzi wako ikiwezekana msevu Jina baya kama vile Malaya, msaliti, mchawi,shetani hii itakusaidia sana kumu ignore
 
Kuna vitu siwezi vifanya mama.. naheshimu private kitu kikitokea sirini usitegemee kukiona wazi!
Ukiniacha nakufa nalo moyoni simtangazii mtu!.. ila nami ukiniacha usifikirie utaniacha tu lzm kuna kitu nikupandikizie moyoni kikisumbue haiwezekani nisumbuke pekee..😂😜
Jinsi nna moyo wa kijasusi, haki sikumbuki last time kuumia kwa ajili ya mapenzi ni lini🤣🤣
 
Sijui Mungu aliniumba na moyo wa aje...!!??
Anyway, pele sana mkuu
 
Back
Top Bottom