Naweza kumtafsiri Zitto Kabwe hivi...

Naweza kumtafsiri Zitto Kabwe hivi...

Gidyflexy

New Member
Joined
Nov 28, 2015
Posts
2
Reaction score
1
Kimsingi Zitto ni mtu anayezingatia zaidi maslahi yake binafisi.

Maslahi binafisi ya Zitto yapo katika makundi mawili.

1. Maslahi binafisi ya kimasilahi(vyeo ama ulaji. HAPA NDIPO HUWATOSA WAPINZANI WENZAKE).

2. Maslahi binafisi ya kisiasa.(HAPA HUUNGANA NA WAPINZANI KATIKA KULINDA POLITICAL STABILITY YAKE).

1. Kitendo cha Zitto leo kutotoka nje nakiona kuwa ni njia ileile ya kulinda maslahi yake ya kiuongozi ama vyeo. Kwa kete hii ataitumia kupata kura nyingi za wabunge wa CCM katika nafasi nyeti ya kamati ya bunge aliyokuwa anaiongoza ama vinginevyo.

anajua kuwa anahitaji kupata kura za wana CCM na hii ndio namna pekee ya kuzipata kwa kuonekana hajamsusia Magufuli katika kupigania haki ya Wazanzibar na hivyo kuwakonga nyoyo wana CCM.

mbinu hii si mpya kuwahi kutumiwa na Zitto kuzipata kura za wana CCM ama uungwaji mkono wa wana CCM bungeni. mtakumbuka wakati wa bunge la 10 Zitto alifanya hivyohivyo mwanzoni mwa Bunge la 10 kwa kujitenga na chama chake chadema wakati ule kwa karibu kila jambo na alifanikiwa kupata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa moja ya kamati na wengine waliofanikiwa kupata vyeo hivyo ni wale tu waliokuwa mawakala wa CCM ambao ni John Cheyo na Augustine Mrema kwa wakati huo. ikumbukwe kuwa nafasi hizo tatu za upinzani zilitakiwa kutolewa kwa Kambi rasmi ya upinzani lakini danadana zikachezwa na kubadilisha na kuwafanya hadi kina Mrema na Cheyo kupata.!!

mfano mwingine mzuri ni mwaka 2010..... Chadema walivyotoka nje kususia hotuba ya Kikwete na walivyokataa kutambua ushindi wa Kikwete Zitto alibaki bungeni!!Angalia ulikuwa muda gani wakati Zitto anafanya hivi, huu ulikuwa muda kuelekea kwenda kupata vyeo vipya vya bungeni( he sided with CCM to win out CCM MPS and he won them).

kwa maslahi ya namna hii ya kutaka vyeo Zitto lazima atakuwa upande wa kutowakwaza CCM ili ajihakikishie kuungwa mkono na wana CCM kwa kuwa wapo wengi.

2. Maslahi ya kisiasa.
Katika maslahi ya kisiasa Zitto hutumia njia hii kuungana na wapinzani na kuwakana CCM.
Kwa nini Zitto hufanya hivi? Zitto hufanya hivi katika kuhakikisha kuwa analinda nguvu yake ya kisiasa na mara nyingi huja kusimama na wapinzani hasa katika mambo ambayo yanakuwa yameteka siasa za Nchi. Inaweza kuwa skendo kubwa kubwa za kifisadi kama ambavyo amekuwa akifanya ama mambo ya migogoro ya viongozi wa kiserikali.

Mfano mzuri ni pale UKAWA waliopotoka nje na kulisusia bunge la katiba na wakaapa kutorejea na hawakurejea bungeni wakabaki kina Mrema na Cheyo, Zitto naye aligomea bunge na hakurudi kama UKAWA. angalia muda(timing). Hapa muda wa bunge ulikuwa unaelekea kwenye ukomo na Zitto alihitaji kulinda nguvu yake ya kisiasa hasa kwa wananchi kwa kuwa ndio wangempigia kura and he won peoples votes, ingekuwa mwanzo mwa bunge wakati wa kutafuta vyeo asingegoma kushiriki lile bunge la katiba.

Kwa namna hii watu wamekuwa wakimchanganya na kushindwa kumwelewa zitto hasa yupo upande gani? Mostly many are not sure which side will Zitto stand, na ndio maana hata alipohojiwa na TBC pale nje ya bunge kuhusu wapinzani kutoka nje alisema "Wametumia haki yao ya kidemokrasia kuonesha protest, haya ni mambo ya kawaida mno kuna nchi zngne wabunge hurushiana ngumi kabisa,kwahyo wako sahihi mana hakukuwa na namna nyngne baada ya barua yao kutotolewa maelezo,na walitii amri ya spika kuwataka watoke nje"

Kama umeelewa niliyoandika jaribu kuchunguza na utabaini..
 
Mbona kwenye kukataa posho zitto hakuungwa mkono na kina lissu??
 
Na chadema kumkubali lowassa kikuwa na maslahi yapi?
 
Kila mtu anautashi wake sanasana anachofanya Zitto kwenye hayo unayomtuhumu ni kuonyesha hayuko ku support ujinga wa wengine. Mbatia alisema uchaguzi wa bara urudiwe halafu akaonekana bungeni tena, watu hao hao jioni yake tena wakataka kurudi kusherekea ufunguzi wa bunge na maraisi akiwemo Dr Shein baada ya kutoka masaa machache what is the point.

Kwa wanasiasa mahiri duniani kilele cha uongozi ni kuingia kwenye inner circles of power iwe kwenye kitchen cabinet ya serikari au hata ukiwa upinzani kutumiwa na Jamhuri kwenye maslahi ya taifa ndani na nje ya mipaka ya Taifa (ukifika huko ina maana sio kwamba unaaminiwa na wapiga kura tu bali hata na wasimamizi wa national interest).

Kwa siasa za Zitto anazofanya sasa akifika huko itakuwa ni kwa kubebwa hana hivyo vigezo despite his satisfactory performance not brilliant on his quest to improve accountability serikarini; the main problem dude doesn't know when to draw the line or when to shut up kwa mfano mambo ya Zanzibar yanakuhusu nini wanasiasa wote wanaojua limitations zao wamewaachia waelewa wa mambo ya muafaka wafanye kazi zao yeye kihere here tu as if the ppl want hear is opinion.
 
Kama huelewi nyamaza. Huyo ndio zitto zuberi wa kabwela anabadilika rangi kama kinyonga usipo mjua utaingia mkenge lakini mwisho wake umefika wasio mjua ni kina kitila mkumbo tu
 
jitazame sana kumuongelea zito kama unamuongelea muuza kahawa kutakuumiza,,,,muulize kafulila,,,,ukawa tukitaka tuwe threat kwa ccm2020 tumpe nafasi zito kinyume na hapo.....shidahhhh
 
Kila mtu anautashi wake sanasana anachofanya Zitto kwenye hayo unayomtuhumu ni kuonyesha hayuko ku support ujinga wa wengine. Mbatia alisema uchaguzi wa bara urudiwe halafu akaonekana bungeni tena, watu hao hao jioni yake tena wakataka kurudi kusherekea ufunguzi wa bunge na maraisi akiwemo Dr Shein baada ya kutoka masaa machache what is the point.

Kwa wanasiasa mahiri duniani kilele cha uongozi ni kuingia kwenye inner circles of power iwe kwenye kitchen cabinet ya serikari au hata ukiwa upinzani kutumiwa na Jamhuri kwenye maslahi ya taifa ndani na nje ya mipaka ya Taifa (ukifika huko ina maana sio kwamba unaaminiwa na wapiga kura tu bali hata na wasimamizi wa national interest).

Kwa siasa za Zitto anazofanya sasa akifika huko itakuwa ni kwa kubebwa hana hivyo vigezo despite his satisfactory performance not brilliant on his quest to improve accountability serikarini; the main problem dude doesn't know when to draw the line or when to shut up kwa mfano mambo ya Zanzibar yanakuhusu nini wanasiasa wote wanaojua limitations zao wamewaachia waelewa wa mambo ya muafaka wafanye kazi zao yeye kihere here tu as if the ppl want hear is opinion.

....nikikusoma aya ya kwanza, halafu nikikusoma aya ya tatu, napata shauku ya kukuuliza na wewe;
what is your point dude?!
 
jitazame sana kumuongelea zito kama unamuongelea muuza kahawa kutakuumiza,,,,muulize kafulila,,,,ukawa tukitaka tuwe threat kwa ccm2020 tumpe nafasi zito kinyume na hapo.....shidahhhh

...apewe nafasi kama nani?!
 
Kila siku mnasema Zitto ni ccm, leo kaamua kuwaonyesha uccm wake mnaanza kulalamika!

Mnamchukia Zitto wakati huo huo mnataka awaunge mkono kwenye maslai yenu.... Mwaka huu mtamkamata uchawi kila mtu.

Ngoja Dr.Slaa naye arudi ili muone mnavyoporomoka Zaidi!
 
Last edited by a moderator:
Mbona kwenye kukataa posho zitto hakuungwa mkono na kina lissu??

Hao hawahitaji kujikomba. Ma dili ya huyo zzk unayajua ndugu yangu au unajisemea? Angalia jinsi ambavyo ccm ilivyo wabeba ACT kwenye kampeni. Weye usione jinsi ambavyo wabunge wanavyo jaribiwa ili wazikatae wakose hata mia ya kuwasaidia kwenye kampeni zao. We, acha tuuu. Usimwamini mwana siasa na haswa ZZK
 
Ukawa mnashida sana.. Zitto mlimtimua na mlishampa majina yote mabaya leo mnataka ashiriki upuuzi wenu wakijinga na utoto. Ni afadhali am-support JPM kwa uwajibikaji wenyetija tunaouona kuliko kumsupport Mbowe na genge lake.
 
Zzk amesababisha mpinzani wa kweli kafulila ashindwe uchaguzi.mpuuzi xana
 
Back
Top Bottom