nguvumali
JF-Expert Member
- Sep 3, 2009
- 4,923
- 1,325
niliutazama Ujio wa rais wa China kwa masikitiko sana na Tangu jana nimekuwa nikiangalia Mbwembwe za kumpokea Rais Obama na Wamarekani wengine kama Kejeli ya wakati wote katika Taifa letu.
Wakuu wetu wametuambia kuwa Urafiki huu ni urafiki wa Kihistoria na hakika utasaidia pande zote mbili.(tunajilisha upepo).....!
Wachina , Wamarekani na mapebari wengine hawaji hapa kwakua wanatupenda au tuna demokrasia yakutilia mfano barani Afrika, bali wanakuja hapa kwakua ni moja ya maeneo machache yenye raslimali adhimu duniani, wanakuja kuweka mirija yao ya unyonyaji na wapo tayari kwa hilo.
Jiulize kwa gharama zote hizi wanazoingia hawa watu ni kwa mapanzi ya dhati kwetu ?
Inaumiza kwakua tunawavika mataji ya maua wanyonyaji wetu, tunawafagilia barabara na kuzipiga deki njia watakazopita, inakera kwakua Mbele ya safari wajukuu zetu watattuona kizazi cha mambulura kama ambavyo sisi tunawaona wazee waliouza nchi hii kwa vipande vya kioo na shanga kuwa hawakuwa makini na wazalendo.
wajukuu zetu watajiuliza mengi watakapokuwa wanasoma kwenye historia kuwa tuliwahi kuwa na dhahabu, Gas, Mafuta na raslimali zingine, watatuzodoa sana.
heri waliotusaliti kipindi cha utumwa na ukoloni hawakuwa hata na uelewa mpana wa mambo kuliko hawa wasomi, wanaojua mambo kwa kina lakini macho na akili zimepofuka na hakika hatutafika.
NIMEWASAMEHE KINA MANGUNGO, NIMESAMEHE WALIOSAIDIA UKOLONI LAKINI HAWA WANAOTUUZA LEO SITAWASAMEHE.