Nawaza sana, nisadieni

Nawaza sana, nisadieni

Second Lieutenant

Senior Member
Joined
Jan 13, 2014
Posts
143
Reaction score
26
Habari wadau,

Mimi ni kijana ambaye nilimpa msichana mmoja mimba ambaye tayari alishakuwa na mtoto but mumewe alishakufaga, Now naishi na huyu msichana but nashindwa kumwambia amlete mtoto wake niishi naye coz familia yangu haijui kama huyu msichana ana mtoto, dispite her differences but nimeamua kuishi naye.

Je ni muda mwafaka wa kuishi na mtoto wake au ampeleke kwa mama yake mzazi anipe nafasi kumlea yeye na ujauzito wake.

Nisaidieni wandugu.
 
bila shaka bado upo kwenye kipindi cha uvulana, utakapofikia level ya uanaume utajua nini cha kufanya
 
huyo mtoto anaumri gani mkuu?? kama mama mkwe wako anamudu kumlea mpelekeni na mmpe sapoti ya kumtunza huyo mtoto.. kama inashindikana mlee tu mkuu. kwani ukipenda boga ukumbuke kupenda na maua yake.
 
Wewe moyoni mwako unajiskiaje?? Kama una amani kuishi na huyo mtoto kaa naye tu,kama hujiskii vizuri wewe acha tu usijilazimishe,mwenye maamuzi yote ni wewe mwenyewe.
 
Km inawezekana kwa sasa mpeleke kwa bibi ake mpk hapo baadae wazazi wako sio tatizo ni kuwaambia tu.
 
Naamini ulijua anamtoto kabla hujazamisha kichwa wazi lako hivyo uliyajua hayo tangu mapema
Na ulikubaliana na hlo
 
Akae na mwanae. Wewe kama unahisia za kuwa mzazi utajua kuwa kumtenganisha huyo mama na mwanaye si vizuri.
Halafu ni kwanini kizazi cha sasa hivi hampendi watoto?

Na yeye ni binadamu amekuja duniani anastahili mapenzi ya baba na mama kama uliyopata wewe. Kwani yeye ndo alitaka baba yake afariki?

Kwa nini sasa akose mapenzi ya mzazi wake kwa sababu tu wewe umempenda na kumpa mimba? Is that even love?
 
Kulea mtoto huyo n.wewe mwenyewe na maamuzi yako na maelewano yako ww n uliye mpa mimba...na kwan ww umeonaje ndan ya moyo wako??? Kumlea au kumtosa
 
Itakuwa vizuri ukimwacha mtoto na mamaye,kama unaweza lakini! Yaani wewe uwe babake ili apate mapenzi ya baba na mama.
 
Kuwashauri wavulana kama wewe ni tabu sana maana mnaishi ndani ya makosa...

Kamwe huwezi kuurudisha ushuzi uliokwisha uchoropoa mbele ya kadamnasi
...
 
Yaani miafrika ilivyokuwa bounded na familia they cant decide against it even if its for good sake mi nakasirikaga sana yaani huwezi kufanya kitu independently yaani kila kitu mama hataki,baba hapendi,mjomba kang'aka,bibi kalaumu.

Wewe kwako huishi na familia be the god of your own heaven.
 
Kua binadamu unaeona mbali kwani hujui Nani atakusaidia hata kukushika mkono uzeeni au zaidi mlee tuu na mungu atakusaidia, kwani huyo mama wa huyo mtoto hato sikia vizuri..
 
Lazima uangalie the best interest of the child nayo ni kukaa na mama yake! Kwanini umtenge mtoto na mama yake? Kwanini mtoto awe stranger kwa mama yake aende wapi sasa. Uwepo wako na mama yake ni faraja na Mungu akuwezeshe kumlea kwa mapenzi kama wakwako mwenyewe na Mungu hatakuacha wala kukupungukia. "UKIPENDA JIPU UPENDE NA USAHA WAKE".
 
Mlee huyo mtoto...Kiislamu mtoto aliyefiwa na baba yake ni yatima tayari...Nyumba yenye baraka ni ile nyumba ambayo yatima analelewa ndani yake. Mlee Mungu atakulipa kheri....
Pia utapata double profit manake mama yake atakupenda zaidi kwa kumlelea mwanae.....atakuthamini.....
 
Hivi kila siku tunaenda kwenye nyumba za ibada kwanini hatuwezi ishi kama tunavyofundishwa katika nyumba hizo.
Mchukue huyo mtoto na uishi nae, faida katika hilo kwanza upendo wa mke/mchumba wako utaongezeka kwako kwa kuona ni mtu unaemjali. Pili, itakusaidia kuwa na utulivu ndani ya familia-waweza mpeleka kuishi kwa mtu akafanyiwa vitendo vyenye kuumiza nafsi (kumbuka mtoto wa kwenye boksi-MORO). Tatu, tunapofundishwa UPENDO huko kwenye nyumba za ibada tunapaswa kuutafsiri ktk maisha yetu ya kila siku.
 
Kama hujui ufanye nini kwenye hili sijui kama unajua kwa nini unaishi na huyo mwanamke!
 
Ukipenda ua utapenda na boga lake
Pia kumlea huyo mtoto kuna baraka sana mfanya awe mwanao awe sehemu ya familia yako
Hakika kautapungukiwa zaidi zaidi utaongezewa
Huyo mwanamke atakuwa real kwako mkuu
Sikiliza moyo wako pia
 
Back
Top Bottom