VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Nipo hapa Dodoma kwa majuma kadhaa sasa. Ni mmoja wa Wanakamati Maalum ya maandalizi ya Mkutano mkuu maalum wa CCM utakaofanyika hapa Dodoma. Mkutano huo utatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu (KK) na Halmashauri Kuu(NEC) ya CCM.
Maandalizi ya vikao vya KK na NEC pamoja na Mkutano mkuu maalum yanakwenda vyema. Nyaraka za baraka bila haraka nyingi zimeshakamilika. Mambo mengineyo nayo yanapangwa na kupangika bila kuvurugika. Ulinzi ndiyo usiseme!
Ajenda yetu itakuwa moja: kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa. Hadi sasa,zijaziona wala kuzisikia fomu za kugombea nafasi hiyo. Nawauliza waandamizi na waamuzi ambao ni viongozi wangu,fomu za kugombea Uenyekiti zinatolewa lini? Tuna siku 9 tu zimebaki!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)