Nawasikia Rais na Waziri Mkuu tuu, wengine kimya

Hii ni Serikal ya Wachapakazi Maneno Maneno peleka Ufipa Mara UKUTA Mara Kata funua lakin kimyaaa!
 
Wako wapi hawa wengine?
Kama tunawaza kuwa kiongozi mzuri ni hadi aongee asikike, tutakuwa tumekosea sana.
Kutawala hadhira kwa kuzungumza ni kipaji cha kuzaliwa na hauwezi kuiga, si wote waliojaaliwa.
Nikija kwenye mada yako, inamashiko tena sana, nitaeleza.
Watu wengi tulitegemea rais na waziri mkuu wanavyoonyesha mfano wa "kufukua madudu", basi na viongozi wengine wote waliopewa dhamana ya uongozi na madaraka, waoneshe kuunga mkono, kama si kwa maneno kwamba hawana vipaji vya kuongea, basi kwa vitendo.
Kuna njia kuu mbili tu za kuonesha mtu anaunga mkono falsafa za kiongozi wake. Ni kwa maneno ama kwa vitendo.
Lakini kwa wateule walio wengi tuliotegemea watakunjurua makucha yao kurarua, wapo kimya!
Wamepewa nyembe na mikasi za kutumbulia, hawawezi kazi hiyo, usaha wa majipu ni vinyaa kwao.
Hata siku1 humsikii karudia ijapo kukariri neno la rais, kama ishara ya kuunga mkono, hakuna. Ni kimyaa.
Wapo viongozi niwataje kwa majina ambao hunistarehesha sana niwasikiapo wakiunguruma. Yupo Lukuvi, yupo Simbachawene, yupo Mbarawa, yupo Naibu waziri wa miundo mbinu, yupo Mwigulu, yupo Naibu waziri wa afya. Hao ndiyo wanaopaza sauti zao kwa mantiki wakaeleweka.
Lakini list iliyobakia ni wengi kwa makumi, kama sikosei baraza la mawaziri wanafika zaidi ya 50! Lakini wamekuwa wapole ghafla!
Upole wanaouvaa si upole wa tabia zao, hapana. Hawa kunakitu nyuma ya pazia, ambapo Rais Magufuli alitakiwa kuwaangalia kwa jicho la pili.
Wapo kimaslahi zaidi. Ni waoga wa lawama kuchukua hatua. Ni wapinzani ndani ya "system", hawakubaliani na uongozi wa juu uliowaweka madarakani.
Kwa kuwa wanalipwa mishahara minono, wanapinga kimyakimya. Hawa kamwe hawawezi kutuletea maendeleo.
Baraza zima tulilitegemea lingetustarehesha kama anavyotustarehesha Magufuli, Majaliwa na wengine niliowataja jinsi wanavyotawala majukwaa wakaeleweka wanachokimaanisha.
Niliona kule Songea sauti ya simba dume inavyounguruma, mumiani wa jasho la wakulima wenye matumbo ya kibepari, walivyotaka kufia "hightable" kwa pressure, walivyogwaya sauti ya mheshimiwa na kuanza mbio kwa mashindano kukimbilia karandinga la polisi kwenda kusokomezwa gerezani.
Nimeona Bariadi pia, Rais Magufuli alivyokataa hadharani bila kumumunya maneno wala kuweka vifumbo taarifa za makandarasi wa majengo nk nk.
Mifano kama hiyo tulitegemea kila kiongozi mahala pake pa kazi abweke, ili kuleta taswira hasa ya kuunga mkono falsafa ya serikali ya awamu ya5.
 
Hao wawili tuu hali iko hivi jeewangekuwa wote namna hiyo pangekuwaje hapa
 
Viwanda viwili tayari cha bakhresa na cha chaki simiyu hongera Raisi na mwijage sijui kaijage
 
Back
Top Bottom