Husika na kichwa cha habari. Nachukua nafasi hii, haswa sikukuu hii ya pasaka kuwashukuru wana JF yafuatayo
1. KUNIPA USHAURI KWENYE
MAHUSIANO YANGU :
Kwa kweli naweza kusema mliniokoa na kifo. Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kukutana na dharau kwa mwanamke nilempenda. Mimi sio mtaalam, ile mada ningeiamvatanisha hapa. Nawashukuru saivi akili yangu imetulia. Yule mwanamke bado yupo kwao na mtoto, bado nipo mwenyewe lakini kwa furaha. Nashukuru mlio ni pm na kunipa soft copy ya vitabu. Nilidownload ndio nakaribia kumaliza kusoma. Kuna waliotoa ya kwao nikajiona mimi nina afadhali.
2. KUNISHAURI KUHUSU KUNGUNI
Kutokana na kuwaza sana, nilishindwa hata kujifanyia usafi binafsi. Mimi ni mfanyakazi wa Umma, lakini Wateja wangu walinishinda hata kuvaa vizur. Kutokana na kushindwa kufanya usafi, KUNGUNI walinivamia. Wwlininyonya damu, asubuhi nimiamka nimechoka. Godoro lilikuw chafu kwa kuwa sikujali.
View attachment 730928
MAKOVU NILIYOBAKI NAYO MPK SASA
(i) Kuzungumza mwenyewe. Hii hutokea niwapo mwenyewe au nikiwa na watu . Huwa najisahau na kusema (mfano) TOKAAAAAA HAPO, nikigundua mtu kaniskia huunganisha na wimbo hata usioeleweka
(ii) Kujisahau sana. Yaani najisahau sana. Naweza hata kuchukua ndoo ya maji kwenda kuoga lakini unakuta nimeigia chooni hadi navua nguo, ndo nashtuka hamna sehem ya kuning'iniza nguo, ndo nagundua
(iii) Kukonda. Suruali yangu ilikuw inabana vizur kiunoni lakini kwa sasa nikivaa surua haikai. Huwa nashonea Suruali kwenye singlendi ili ining'inie vizur kiunoni
(iv) Uume kupungua urefu. Kwa sasa uume wangu umesinyaa tofauti na mwanzo. Asubuh nikiamka wala hausimami tena, labda mara chache. Nilikuwa naenda hadi goli 3. Lakini toka huyu aende nimewahi kutoka mara 1 lakini goli moja mpk asubuh. Tena goli dhaifu la sekunde ya 40 hivi. Nilisingizia naumwa tumbo siku hiyo.
(v) Kucheza dansi mwenyewe. Hii hutokea tu napokuwa chumbani mwenyewe, au nikiingia bafuni nikivua nguo huwa nadansi ile mbaya.
(vi) Kutokupenda kula
KWA NINI YOTE HAYO?
Sikutegemea kuwa nyuma mpk sasa kwa sababu ya MAHUSIANO (mwaka wa 4 nafanya kazi maendeleo hamna ). Imefika mahali natamani kuuza kiwanja changu!
SHUKRANI
Ile hali ya kujiuwa haipo tena, kwa sasa natamani maendeleo.Pia nimeacha pombe(hii ni hatua kubwa kwangu) Nawashukuru wana JF kwa ushauri wenu. Japokuwa ilifika mahali nikashindwa hata kufanya kazi, hadi nikaingia kwenye madeni makubwa, mpk sasa nadaiwa laki nne na elf ishirini (420,000)
Naendelea kulipunguza naamini litaisha. Najibana sana.
Mungu awalinde wana JF, nawapenda , pasaka njema, msherekee salama