Kumekuwa na maoni tofauti na mijadala mingi tangu itangazwe rasmi kuwa Sumaye anawania uenyekiti wa kanda ya Pwani Chadema. Eti watu wanasema 'toka uwaziri mkuu hadi eunyekiti wa kanda'. Hapa wanataka kuonyesha ameshuka daraja.
Wapotoshaji hawa hawajiulizi hivi uenyekiti wa kanda ni ukuu wa mkoa? Angeshuka daraja kama angepewa cheo cha kiserikali kama ukuu wa mkoa na akaukubali. Mbona hawamshangai Kikwete kutoka rais hadi makamu mkuu wa Chuo? Hivi wanajua malengo ya Sumaye kisiasa? Au ni wivu tu wa kuona mtu mkubwa kama Sumaye anaenda kufanya active politics na Chadema? Au wanaoshangaa ni wale waliozusha propaganda za Lowassa na Sumaye kurudi Ccm?
Waliodhani mawaziri wakuu hawa wanabip wamechelewa kukata tamaa. Hawa wamedhamiria haswa kuanzisha himaya kubwa ya kisiasa nje ya Ccm. Subirini muone!