Kuna mtandao fulani umezaliwa ndani ya awamu ya tano, hauna nguvu ndani ya CCM, una nguvu katika mawasiliano binafsi ya nje ya chama.
Ni mtandao mbaya kama ule wa enzi za JK na mzee wa Monduli, kwani siku zote mnapounda kundi ndani ya kundi hamuwezi kuwa na ile roho ya umoja, mtaongozwa na ubinafsi uliojificha.
Lakini iwapo Mungu aliweza kuwafanya watu wa Babeli wakaongea lugha tofauti japokuwa ni wamoja, hatashindwa kuusambaratisha huu mtandao mpya wenye kufurahia kuona mtu fulani akiwa anateseka (sadism).