Nawaonea wivu ambao wameshaoa

SAYANSIKIMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2014
Posts
1,132
Reaction score
260
Nipo hapa usingizi haupo kabisa.

Tamaa zimewaka vibaya mno natamani namimi ningekuwa nimeshaoa tayari lakini umri na uwezo wa kiuchumi hauniruhusu kufanya swala hili haraka iwezekanavyo kama ningekuwa na uwezo ningejiongezea miaka na uwezo wa kiuchumi ili kufanikisha swala hili haraka iwezekanavyo maana naona suala linakwenda taratibu mno .

Acheni tu kipindi hiki kinaniwia ugumu mno kumbe mapenzi yanatesa moyo kiasi hiki.

Maana nipo hapa nimepanga kwenye chumba kimoja niko peke yangu .

Kwa kweli mapenzi ni kitu kingine kabisa.Ngoja nivumilie ipo siku nitampata tu wa kufurahisha moyo wangu.
 
Acha visingizio, kwako umri sio kigezo..kama umepanga chumba, inaonekana ni mtu unayefanya kazi, una akili timamu na unajitegemea..hivyo ndo vitu vya muhimu kwenye kufanya maamuzi ya kuvuta jiko, na wala si miaka.
 
Chumba Kweli nimepanga lakini sio mfanyakazi ni mwanafunzi wa chuo mpaka kuja kumaliza masomo, kutafuta na kupata kazi, kujenga nyumba yangu na kuwa na uwezo wa kujitegemea nimekadiria ni kama miaka 9 Ijayo.
 
Hadi ujenge NYUMBA?!!! Hivi kila alieye oa amejenga? Kwa mishahara ya Tz utasubiri sana!
 
halafu maisha bana kuna wengine iliwafanikiwe au wafilisike ni lazima waoe
 
Ukiweza kununua sufuria moja we vuta Mamsap ndani vingine vitakuja vyenyewe
 
Waliopo ndani wanatamani kutoka nje na waliopo nje wanatamani kuingia ndani.
 
Angalia tu tusije kuona kwenye magazeti ya Shigongo umebaka kuku au mbuzi...
 
We si ulisema ulipataga mchumba humu mmu? uchumba uliishia wapi?
 
Kumbe ushagundua yote hayo bado alafu unataka kuishi kesho angali uko leo?
 
Chumba Kweli nimepanga lakini sio mfanyakazi ni mwanafunzi wa chuo mpaka kuja kumaliza masomo, kutafuta na kupata kazi, kujenga nyumba yangu na kuwa na uwezo wa kujitegemea nimekadiria ni kama miaka 9 Ijayo.

Kama ushagundua bado miaka yote hiyo pambana miamko ya mwili uyashinde maana miaka 9 si lele mama
 
Oa tu umri sio tatizo na pia kuoa si lazima uwe na nyumba
 
Jana tu hapa alikuwa anasaka mchumba!
unataka kuoa na unasoma? Wewe kweli sayansi kimu. Hebu soma acha udwanzi

Ndoto nyevu zinamsumbua masikiniii......amwombe ushauri yule Albo nani sijui....amshauri jinsi ya kuscore goli mbili ndotoni baada ya kula ugali na matembele.
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…