TEKNOLOJIA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 4,305
- 2,563
Nikiwa miongoni mwa Watanzania tunaopenda kufuatilia muziki wa nyumbani nimetokea kuvutiwa na wasanii mbalimbali wanaofanya genres tofauti tofauti za muziki kama vile hipohop,rap,r&b,pop,housing, rock,dancehall, nk.Miongoni mwa wasanii niliotokea kuwakubali sana kwa miaka ile ya 2000 kurudi nyuma ni Jay Moe,AY,MwanaFA,Inspector Haroun,Juma Nature,Solo Thang,Mapacha,Lady Jay Dee,Mad Ice, Ngwair, nk.
Katika miaka ya karibuni kimezuka kizazi kipya cha wanamuziki ambao nawakubali kiasi kwa mfano lile kundi la zamani la Nako 2 Nako lililoundwa na akina G Nako,Ibra da Hustla,Lod eyes,Joh Makini. Pia kuna akina Belle 9,Ben Paul,Jux,Diamond, Ali Kiba,Vanesa Mdee, nk.Lakini hata hivyo nimetokea kuguswa sana na muziki unaofanywa na kundi la Navy Kenzo linaloundwa na wasanii wawili yaani Aika na Nahreel.
Nimekuwa nikiwafuatilia hawa jamaa tangu walipokuwa na kundi la Pah One, kusema kweli wanafanya muziki tofauti sana na wenzao, hata ukicheki videos zao utaona jinsi ambavyo walivyo more professional, videos zao zimetulia sana, nyimbo zao zinavutia sana kiasi kwamba utatamani ufuatishe kila mstari wakati wimbo wao unapokuwa hewani,in short jamaa wanajua wanachokifanya.
Kama wewe ni mpenzi wa muziki mzuri usiyependa kufuata mkumbo utakubaliana nami kwamba kwa hapa bongo Navy Kenzo ndio wanaofanya muziki unaoeleweka zaidi yaani club hits au club bangers, Kinachonivutia zaidi kuhusu Navy Kenzo ni kwamba huwa wanasimama wenyewe tu,hawahitaji collabo za wasanii maarufu wa ndani ya nchi au nje ya nchi kutengeneza muziki mkali kama wanavyofanya wasanii wengine hapa nchini.
Asanteni na ninawatakia Pasaka njema.