Nawahi kushiba Kila ninapokula chakula

Amos David Mathias

JF-Expert Member
Sep 3, 2022
1,574
3,029
Wakuu poleni Sana Kwa usumbufu naweza sema JF nimekuwa mtu wa kulalamika Sana.Kwanza napenda kuwatakia wote ambao mna afya migogoro uponyaji Toka Kwa muumba na tulizo la Moyo kwenu.

Wakuu nimekuwa mtu wa kula chakula kidogo sana Kisha nashiba naacha chakula kingi kinabaki.Sahani ya wali ya shilingi Elfu Moja ya wali maharage huku Dar es Salaam naiona nyingi Sana.Naishia kula robo nikijitahidi Kwa kujilazimisha ndipo naishia kumaliza nusu ya wali nilionunua mwingine namuachia waiter akaumwage naulipa naondoka.

Nashangaa Sana watu wanaoagiza chakula kingi na kujishangaa zaidi Kwa hali niliyonayo.Lakini pia Nina dalili hizi;

# Pindi baada ya kula na kushiba basi nashiba muda mrefu sanaa ingawa nimekula kidogo

# Tumbo linakuwa linauma na limejaa Kwa kuangalia Kwa macho limevimba

# Maumivu makali ya tumbo

#Nakosa choo hata wiki Tatu kawaida na nikija kupata choo kinakuwa kidogo sana tofauti na nilichokula

# Maumivu makali ya mgongo kama vile mtu ananiunguza na maji ya moto hasa mgongo wa juu maumivu haya nimeishi nayo Miaka mitatu tangia nianze kuyapata
Nikikalia sofa na kuliegemea mgongo unauma.Siwezi lalia mgongo sababu utauma.Maumivu haya ni ya Kila muda Kila siku Kila wakati.Japokuwa nikiwa natembea au nafanya kazi yanapotea ila nikikaa chini nikaegemea sofa yanaanza.Nikikalia viti vya plastiki ndyo yanakuwa Kwa mbali.

Mara nyingi maumivu haya mida ya usiku ya kulala yanakuwa makali Sana.Hivyo nalazimika kununua bando angalau niingie mtandaoni kujipooza maana usingizi nakosa kabisa.

#Nimepungua uzito Sana.

# Ikifika mida ya kula nakosa appetite au naanza uvivu kula.

Kwa yeyote aliyewahi pitia hili jaribu akalishinda tusaidiane.

NB:YOTE HAYA YALITOKANA NA KUENDEKEZA MAWAZO NA STRESS.
 
Unataka tupige ramli? Nenda hospital kwa vipimo na matibabu sahihi.
Pole.
 
Kumbuka Pesa Inaogopa Njaa.

Hivyo Basi Mkuu Hizo Ni Dalili Za Kibunda Mfukoni Kimeanza Kuongezeka.

Pesa Ikiongezeka Unakula Kwa Hamu/Radha Si Kushiba Hivyo Unajikuta Unakula Kiasi Cha Kawaida Tu Na Unaridhika.


Ngoja Tunasubiri Wataalamu Watupe Muongozo Wa Afya.
 
Back
Top Bottom