Nauza barbershop

Nauza barbershop

Lashaini

Member
Joined
Nov 4, 2011
Posts
74
Reaction score
60
Ipo sinza sehemu nzuri,sema ninafanya kazi mkoani ivyo usimamizi umekua mugumu kwa nyoyote atakae itaji tuwasiliane 0653441748
 
Milion 15 inajumuisha nini kiongozi? kodi inaisha lini? sinza sehemu gani? au ndo unataka kumbambika mtu, madalali nyie hata kwa mtogole mnaita sinza
 
Ipo sinza sehemu nzuri,sema ninafanya kazi mkoani ivyo usimamizi umekua mugumu kwa nyoyote atakae itaji tuwasiliane 0653441748

mludishie nwenyewe frem yake kama umeshindwa biashara,na hivyo vitu vyako ufungue huko mkoani hiyo barber shop.
 
Weka tarifa muhimu zingne wana jamvi, kama sinza ipi? Pango inaisha lini? Thaman za ndan zipoje? Ebu weka sawa
 
Weka taarifa muhimu
Frame ya nani?
Kodi ya mwezi ya frame ni ngapi?
Wewe umelipa hadi lini?
Ina vifaa gani ndani ambavyo ni Mali yako?
Sinza sehemu gani?

We kuwa Mkoani si taarifa muhimu kwa manunuzi, maana mashine ya kunyoa haiwezi kuwa Milioni 15! Jaribu kujustify hiyo Milioni 15 na kuvutiwa zaidi ikiwezekana mapato ya wastani kwa mwezi na hata Changamoto za hiyo biashara.

Watanzania tutakuwa wababaishaji hadi lini? Tunawafundisha kila siku lakini hamelimiki.
 
Mie nijuavyo Salon ya kiume inajisimamia yenyewe kwa kiasi kikubwa hata uwe mkoa gani.
Maana ni kama Daladala hesabu ya siku inajulikana na pia katika vinyozi huwa anateuliwa mmoja kama kiongozi na ndio hukabidhiwa pesa na vinyozi wengine ili akutumie na kusimamia mambo madogomadogo ya Salon.

Kwahiyo sidhani ni sababu kubwa ya kuacha hiyo biashara kama inamlipa na kama inakidhi ushidnani wa salon za Sinza.
 
Ipo sinza sehemu nzuri,sema ninafanya kazi mkoani ivyo usimamizi umekua mugumu kwa nyoyote atakae itaji tuwasiliane 0653441748

Mkuu, mimi naishi Sinza, hiyo Berbershop itafaa, ni-PM tuongee biashara. Lakini zingatia maswali yafuatayo:-

1. Frame iko sehemu gani hapo Sinza
2. Ina ukubwa gani
3. Ndani yake umeweka vitu gani?
4. Una wafanyakazi? Wangapi?
5. Mkataba uliopo ukoje? Kodi yako unalipa kiasi gani na lini inaisha?
6. Je wewe ndiwe mpangaji asilia au na wewe umechukua kwa mtu aliyepangishwa?
7. Hiyo Milioni 15 Iinahusisha vitu gani?
8. Unalipa kodi TRA? Unadaiwa? Leseni halali?
9. Vipi kuhusu maji na umeme?
 
Kama upo mbali na unashindwa kusimamia na wateja wapo sehemu hio jaribu kuingia mkataba na hao vinyozi, wawe wanakupa rent / mapato kwa siku..., mfano kila kinyozi elfu 5,000/= kwa siku (au bei yoyote kulingana na wateja wa hapo)

Hio itakusaidia wewe kuepuka mambo ya usimamizi sababu vitu vikiharibika ni wenyewe..., umeme wawekee luku wawe wanalipa wenyewe. Kwahio wewe kazi yako itakuwa ni kuwabana pesa ya siku. Na sababu upo mbali waambie wawe wanakurushia mmpesa daily na kama unamjua mtu karibu hapo awe anawatembelea na kuwabana wale wasiotuma pesa yako.
 
Asante kwaushauri wenu mzuri,baada ya kuufwata naona mambo yanaenda vizuri atawazo la kuuza limeondoka nashukuru sana
 
Back
Top Bottom