Nauza bajaj niliyoichukua kwa mkopo, atakayeitaka atatakiwa kurudisha rejesho

Ni nouma!
 
Ni biashara kichaa ofcoz..maana service zote pia ni juu yako.
 
Wakati bajaj hesabu kwa siku ni 20,000 sawa na 140,000 kwa wiki ambazo zote ndio ukalipe deni je service utafanyaje au kukiwa na matengenezo ya dharura itakuwaje!
Matatizo mengine ni ya kujitakia tu.
 
Rejea post ya mtoa uzi Kuna 1m amesha toa tayari je atarejeshewa akishamaliza mkopo?
Pia kumbuka rejesho ni kwa wiki si kwa mwezi. Hivyo miezi 24 ni sawa na majuma 52 x 2.
Kwa hivyo hesabu hesabu sahihi ni:
Tsh 139400 (rejesho la kila juma) x 104 (majuma ktk miezi 24) + TSh1,000,000 (downpayment) = Tsh 15,497,600. Pesa inatosha kununulia IST kabisa.
 
Yaani kwa siku dereva anatakiwa kuhakikisha anapata 20,000/= ya marejesho! Na zoezi hilo linatakiwa lifanyike kwa miaka miwili mfululizo!!

Si mchezo.
 
Khaaa jamaa aingize elfu 30 kwa siku labda ndo itawezekanaa sasa bajaji elfu 30 kwa siku utaitoa wapi??? hapo hujalaa..mafutaaa pia.
Unashangaa dereva Bajaj kuingiza Tsh 30,000/= per day?hiyo hela hata bodaboda wanaofanya kazi yao kwa umakini ni ndogo wao kwa siku wanafunga siyo chini ya 50K kinachowaangusha ni wanawake hakuna cha zaidi.

As for me,huo mkataba ni rahisi tena rahisi sana changamoto anazipata jamaa kutokana na hakukaa akapiga hesabu zake vizuri wapi itafanya kazi au dereva siyo muaminifu etc,Bajaj wanapata hela kwa siku kulaza 60K chuma ikiwa full tank ya kuamkia kesho na hesabu ya boss ameshatoa ni ishu ndogo sana,75% rout zangu nazozunguka town natumia usafiri huu so nimekuwa nauliza uliza sana kwa madereva na ndicho wanachoniambia.

Mimi nafanya hii biashara,nimeianza 2020 kipindi kile kwa siku ilikuwa 20,000/= mkataba miaka miwili mwaka jana mwishoni nikapandisha 25,000/= sasa piga hesabu hapo inakuwa bei gani na hela wanaleta,Bajaj hasa hizi TVs ni chombo kimoja imara sana mtu akifanikiwa kumaliza mkataba ana miaka nane mbele hata zaidi kukimiliki kikimuingizia hela na service yake kwa siku 18 haizidi 27K.

Engine yake kwa mtunzaji mzuri kuanza kumsumbua ni kuanzia miaka sita so mara nyingi faida wanaipata zaidi madereva ila wale wanaojitambua.
 
Fikiria uwepo wa mvua Kuna kuumwa hao wakopeshaji na makatili Sana japo mkopaji hakuzichanga vema
Uwepo wa mvua Bajaj na pikipiki hiyo siku ndiyo sherehe yao wanapiga hela mbaya kabisa,kinadada na mabishoo wanaogopa madimbwi so wateja wanaongezeka.

Kuumwa (siujui mkataba wa huyu unasemaje) ila mingi hiki kipengele kipo kwamba siku hiyo itolewe kwenye hesabu au atafutwe day worker apige kazi.
 
Jamaa apige Route ya Lami asiipelekea makorokoroni itawahi kuchokaaa.. Na kama yupo dar nahisi inakuwa simple.
 
sipingani na ulichokisema na uwezekano wa kuirejesha upo ila angeongeza hela achukue zile za bank za mwaka mmoja. Hizi angalau kidogo 24 months sio poa japo bajaji inahitaji nidhamu ya hali ya juu ukipata dereva msumbufu unaweza ichukia hii biashara.
 
Ni nouma!
Tatizo mdau umeingia wenge mapema,hiyo chuma ni yako kama unaendesha mwenyewe tatizo sijajua kama na wewe umempa mtu,ingekuwa umeinunua kwa cash yako ningekushauri um'bane kwa vifungu.

Kama umempa mtu ndiyo itakuku-cost kutokana na wengi siyo waaminifu ila kama unayo mwenyewe sogea maeneo yenye watu utafanya kazi hela utapata nidhamu yako tu inahitajika.
 
sipingani na ulichokisema na uwezekano wa kuirejesha upo ila angeongeza hela achukue zile za bank za mwaka mmoja. Hizi angalau kidogo 24 months sio poa japo bajaji inahitaji nidhamu ya hali ya juu ukipata dereva msumbufu unaweza ichukia hii biashara.
Hizo za benk bahati mbaya unakuta siyo wengi wanaojua ndiyo maana kama hivi mtu anajipiga pin.

Nilipo-bold,umesema kweli hata mimi dereva wa kwanza nilieanza nae alinichanganya kiasi nikaona hii siyo kazi,kwanza simu hapokei akipokea anakwambia yupo garage chombo kimesumbua (ina miezi minne tu Bajaj mpya) niki-check GPRS inaniambia inatembea eneo fulani,nilivunja mkataba na hela yangu 500K akabaki nayo.
 
Nimesoma maelezo yako. Ila situation ya jamaa ngumu. Apige kazi ili arejeshe mkopo kila wiki, hapo bado hajaweka fedha ya matumizi (ukute ana familia pia), pia gharama za uendeshaji bila kusahau siku mbaya kibiashara. Hii biashara inaweza kuwa reasonable kama angenunua cash na awe anafanya biashara mwenyewe. Katika vitu vingi vinavyofanya biashara nyingi za Bongo zife ni uaminifu wa wafanyakazi!
 
Kwa uzoefu wako. bajaji aina gani ni nzuri kwa biashara? Ukinunua mpya, fedha yako inarudi baada ya muda gani baada ya kuondoa gharama za uendeshaji (eg, service, mafuta, traffic) na matumizi yako binafsi kama unaendesha mwenyewe?
Nitakujibu kwa kuzingatia hapo nilipo-bold.

Bajaj nzuri ni TVS,ukiinunua mpya kwa sababu unakuwa hauna tajiri kinachopatikana chote ni cha kwako assume hela yako inarudi baada ya mwaka mmoja (nimesema hivi sababu aliyenishauri alinunua ya kwanza akawa anaendesha mwenyewe baada ya mwaka akatoa mpya so faida ilinunua chombo kipya) kwa wewe usiye mzoefu fanya mwaka ½.

Bajaj haina service kubwa (labda ufungue engine na engine za TVs chini ya miaka mitano haisumbui) service zake ni ndogo ndogo tu ambayo ni kila baada ya week tatu haizidi 30,000/=
 
Hii bajaji naamini ni nzima haina tatizo isipokuwa hilo deni. Kwanini ulikubali kulipa sh. 139,400 kwa wiki. Hakuna kazi ya kupata hizo pesa na wewe ukala ugali. Anayeitaka aende akabadili mkataba. Makampuni ya kinyonyaji yanaingia sana Tanzania sasa hivi. Mara unauziwa vyumba juu ya ghorofa unaambiwa ni nyumba yako. Ukinunua humalizi deni na huwezi kufuga hata kuku. Ukishindwa wanachukua na vya kwako vyengine na pesa hawarudishi.Angalieni sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…