Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,856
Hivi nchi hii bila upinzani leo hii hali ya mtanzania na Taifa kwa ujumla ingekuwaje?
Ni bahati mbaya sana swala la kukosoa serikali na kutoa mawazo mbadala kwa kiasi kikubwa limeachwa kwa wapinzani tena huku wakati mwingine mawazo yao yakibezwa!
Japo upinzani uko Bungeni na Bunge ni mhimili mmojawapo wa dola,lakini upinzani ndani ya Bungeni ni kama chombo kinachojitegemea ambacho wakati mwingine hulazimika kuhamishia shughuli zake nje ya Bunge kutokana na uchache wao na kutoungwa mkono na walio wengi ndani ya Bunge.
Upinzani nchi hii umefanya kazi kubwa sana ndani ya Bunge na nje ya Bunge kiasi kwamba leo nauona ni kama mhimili wa tano wa dola baada ya vyombo vya habari.
Mtawabeza,mtawadhihaki,mtawakejeli, lakini kamwe hamtabadili ukweli huu.