Uchaguzi wa 2015 si muda mrefu utaiweka Tanzania ya leo pahala pake panapostahiki. Kwa muda mrefu viongozi walijificha chini ya kapeti na sioni aibu kusema kuwa waliihadaa dunia kuwa Tanzania ni nchi ya demokrasia na inayojali haki na usawa.
Ya Zanzibar na yanayoendelea ni mwendelezo tu wa mgogoro uliofichwa chini ya uhafidhina wa watawala wa Zanzibar wanaoungwa mkono na Tanganyika kwa mwavuli wa Chama(CCM) na muungano. Ni mgogoro ule ule wa kisiasa wa tokea kuja siasa za vyama vingi wa kutokubali kuachia madaraka kwa njia za kidemokrasia.
Siasa hizi zimeleta mpasuko na mgawanyiko wa kasi na tayari umejenga zama mpya za uadui wa kisiasa katika mazingira ya kikatiba yanayotambuwa umoja wa kitaifa na mashirikiano. Hali hii itakuwa ngumu sana na italeta utawala wa kulazimishwa kwa nguvu kushiriki katika uongozi hata kama unafanyiwa faulu. Jee hili litawezekana kama wanavyotaka watawala (CCM)? tusubiri tuone
Nauona Mgogoro na zama mpya za siasa chafu hapa Tanzania na Zanzibar yake baada ya matokeo ya huo uchaguzi wa marudio.
Naiona nguvu kubwa ya mtawala kutaka kulazimisha utawala wake uheshimike hata kama wananchi walishaukataa kupitia uchaguzi huru na haki wa Oktoba,2015.
Nauona mtanziko wa kisiasa na hujuma, kuwekana ndani na visasi.
Naiona Tanzania ikiporomoka katika anga za kidiplomasia na kukosa ushawishi katika dunia.
Naiona Tanzania ikiwekewa vikwazo vikubwa katika historia yake na kudhoofika kwa maendeleo na muungano wetu. Hapa nitoe maelezo kidogo
Kwamba ikiwa jumuiya ya kimataifa itaendelea na msimamo wa awali ni dhahiri Tanzania haiwezi kushindana na Mataifa makubwa na fitina za nchi kubwa ni mbaya na zinaweza hata KUHATARISHA muungano wetu. Wazungu wana ufunguo wa Muungano wetu huu wa pekee na kwa joto la Zanzibar linavyokwenda huko mbele kuna hatari ya kutikisika muungano na maendeleo yetu.
Nauona utawala wa kiimla na mgawanyiko wa kijamii huko Zanzibar. Naiona Tanzania inayoyoma kusikojulikana naiona Zanzibar inazama dididi.
Ikiwa mataifa makubwa ya kizungu na marekani zimesusa na kinachoendelea Zanzibar tumejitayarisha vipi na fitina zao? jee leo hii hatuwahitaji tena wazungu ? tunao ubavu huo? ngoja tuone
Suali lengine hivi iwe tu kwamba CUf wamekaa kimya na hawajui kinachoendelea mbele?
Masuali haya yananitia woga na kuhitimisha kwamba bado Nauona mgogoro mkubwa wa kisiasa Zanzibar.
Hatufurahii lakini ukiomba mvua itakunyeshea. Mungu atuhidi