wegi wanafuata mkumbo wa mawazo hawajui siasa ya Tanzania na hasa siasa ya CDM, wanamuandama zzk kwasababu fulani anampinga bila kuwa na mtazamo chanya. Tumefungwa fikra na viongozi wa CDM tumekuwa wendawazimu.
Na Mwandishi wetu - Imechapwa 18 November 2009 SHIDA Salum, mama mzazi wa SHIDA Salum, mama mzazi wa
Naibu Katibu Mkuu wa Chama
cha Maendeleo na Demokrasia
(CHADEMA), Zitto Kabwe,
ameibuka na kusema mwanaye
anatumiwa kukivuruga chama chake. Akizungumzia taarifa
zinazoandikwa na baadhi ya
magazeti kuhusu kinachoitwa
mgogoro wa uongozi katika
CHADEMA, kati ya Zitto na
viongozi wenzake, Shida alisema, hakuna mgogoro pale,
kuna kikundi cha watu
wanaotaka kumtumia
mwanangu kufanikisha mambo
yao. Akizungumza na gazeti hili juzi
jijini Dar es Salaam, alidai kuna
watu walio nje ya CHADEMA
wanakula njama za
kumgombanisha mwanawe na
viongozi wenzake. Alisisitiza, kuna baadhi ya
wanasiasa ndani ya CHADEMA
wanaotumiwa na walio nje
kugombanisha viongozi. Akaongeza, Mambo ya
uchaguzi yalikwisha kitambo na
Zitto kwa moyo mmoja
alikubali kumaliza tofauti zake
na Mbowe (Freeman Mbowe)
ndiyo maana akamuacha Mbowe kuwa mgombee pekee
wa uenyekiti. Shida aliwatuhumu watu walio
nje ya CHADEMA akisema ndio
wanaopandikiza mbegu za
chuki kwa lengo la kuwavuruga.
Hata hivyo, hakuwataja. Alisema kila mwenye akili
timamu anajua kinachotafutwa,
na nani mkweli na yupi
anasingiziwa. Angalia wanaoandika haya.
Kweli Zitto anaweza kutetewa
na magazeti ya Habari
Corporation yanayomilikiwa na
Rostam Aziz halafu ukaamini
kile kinachoandikwa? alihoji. Aliongeza, Rostam yupi? Ni
huyu tunayemjua au mwingine?
Kwa wema upi alionao kwa
chama chetu. Wiki iliyopita magazeti ya Rai
na Mtanzania yalinukuu taarifa
zikidai kuwa zimetolewa na
Shida, kwamba anataka
mwanawe aondoke kwenye
chama hicho kwa kile ilichoeleza kuwa
kumwepuesha na yaliyomkuta
Chacha Wangwe. Katika kujibu hilo, Shida
anasema, Mimi na Zitto tunajua
katiba ya chama chetu.
Tunafahamu taratibu za
kuendesha chama. Yeye ni naibu
katibu mkuu, mimi ni mjumbe wa Kamati Kuu. Tunajua nini
maana ya uongozi, hivyo
hatuwezi kukurupuka
barabarani. Kwamba kama kuna
malalamiko au tuhuma
mathalani juu ya uteuzi wa
wabunge wa viti maalum, basi
sote ni sehemu ya hicho
kinacholalamikiwa. Kutokana na hali hiyo, hatuwezi kujifanya
hatuhusiki na tukatuhumu
kupitia vyombo vya habari, tena
magazeti yanayomilikiwa na
mwanachama wa CCM. Shida alisema anajua kwa
mapana chanzo cha yote
yanayoandikwa na jitihada za
kutaka kumgombanisha Zitto na
viongozi wenzake, hasa Katibu
Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa na mwenyekiti
wake, Freeman Mbowe. Yote haya tunafahamu chazo
chake. Si uchaguzi wa ndani ya
chama. Uchaguzi ulishakwisha
na Zitto kwa moyo mmoja
alikubali kumuachia Mbowe
uenyekiti ili kulinda maslahi ya chama, alisema. Alisema kuwa yeye kama mlezi,
hawezi kuruhusu hali hiyo,
hivyo atatumia nafasi yake ya
mjumbe wa CC kuhakikisha
kwamba tabia hiyo ya
kugombanisha viongozi inakoma. Nikiwa mzazi, mlezi na
mjumbe wa kamati kuu ya
CHADEMA, siwezi kuruhusu Zitto
kutumika kuingiza chama
katika mgogoro. Nitasimama
imara kuhakikisha kwamba CHADEMA inakuwa salama,
alisema. Wiki iliyopita, Dk. Slaa
aliwaondoa katika nafasi za
utendaji David Kafulila
aliyekuwa Afisa Habari na
Danda Juju aliyekuwa Afisa
anayeshughulika na Halmashauri na Bunge kwa kile
kinachoelezwa kuwa utovu wa
nidhamu kwa chama na
viongozi wake. Kafulila alinukuliwa na baadhi
ya magazeti kuwa alibeza kikao
cha viongozi wa juu wa chama
hicho kilichofanyika Dodoma
ambapo Mbowe na Dk. Slaa
walikutana katika kikao cha kawaida na wabunge wa
chama hicho na baadhi ya
wakurugenzi. Kafulila alisema mkutano huo
wa viongozi haukuwa na
maana; na alifika mbali zaidi
kwa kuufananisha na vikao vya
geto. Ni matamshi hayo na
mengine yaliyomfanya Dk. Slaa kutumia mamlaka yake ya
kikatiba kumuondoa Kafulila
katika wadhifa huo. Taarifa zinasema hoja ya
kumuondoa Kafulila katika
kikao ilitolewa na Msafiri
Mtemelwa, mmoja wa viongozi
wake na ambaye alikuwa
meneja wa kampeni za Zitto wakati wa kuwania uenyekiti
wa CHADEMA.
Suorce: MwanaHALISI.