Naunga mkono Zitto kuwania urais - Kigwangalla | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naunga mkono Zitto kuwania urais - Kigwangalla

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 1, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Na Suleiman Abeid, Shinyanga | Majira

  MBUNGE wa Jimbo la Nzega mkoani Tabora, Dkt. Hamis Kigwangala, ametangaza kuunga mkono dhamira ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Zitto Kabwe, ya kutangaza kuwania urais mwaka 2015.

  "Naunga mkono Bw. Zitto kwa dhamira yake ya kutaka kuwania uongozi wa juu kabisa katika nchi yetu japokuwa yuko CHADEMA na mimi niko
  CCM," alisema Dkt. Kigwangwala.

  Dkt. Kigwangwala alitoa kauli hiyo alipokuwa akiwahutubia wanafunzi wa Sekondari ya Shinyanga, iliyopo wilayani Kishapu mkoani hapa, wakati wa mahafali ya 46. Katika mahafali hayo, Dkt. Kigwangwala alikuwa mgeni rasmi.

  Mbunge huyo alisema vijana wanaomaliza masomo yao wasipokuwa na malengo ya kuwa viongozi wa nchi itakuwa hatarini kujikuta ikikosa vijana makini.

  Hapo ndipo alipotolea mfano Bw. Zitto, akisema alisoma naye shule moja, ambapo tangu akiwa masomoni alikuwa na ndoto ya kuwa kiongozi.

  "Binafsi nampongeza kijana mwenzagu Zitto (Kabwe), maana tangu tukiwa shuleni alikuwa na malengo ya kuwa kiongozi, sasa hivi ametangaza nia yake ya kutaka kuwania urais wa Tanzania mwaka 2015, ameniwahi hata mimi natamani siku moja nitakuwa rais, lakini leo hii hapa sitangazi nia hiyo," alisema Dkt. Kigwangwala na kuongeza;

  "Muda wake bado, ipo siku nitatangaza dhamira hiyo, akijitokeza kijana nitamuunga mkono...kwa hiyo namuunga mkono Zitto kwa dhamira yake ya kutaka kuwania uongozi wa juu japo naelewa hawezi kutushinda CCM."

  Ili taifa liendelee kupata viongozi, Dkt. Kigwangwala alisema hakuna sababu ya vijana waliopo mashuleni kubaki na dhana kuwa masuala ya siasa yanahusu wanasiasa waliopo madarakani au watu wazima peke yake, badala yake waanze kujiwekea malengo yatakayowawezesha kushika uongozi wa nchi.

  Aliwataka vijana watakaobahatika kuingia katika siasa na kupata nafasi za uongozi kujiepusha na siasa za makundi ambazo hivi sasa zinaitafuna nchi.

  "Epukeni makundi yanayohujumu Serikali na hatimaye kutaka uongozi wa nchi yetu, hakikishesni mnawakwepa wanasiasa wa aina hiyo, maana hawafanyi siasa kwa malengo ya jamii, hawafanyi siasa kwa malengo ya umma wanafanya siasa kwa malengo ya kutunisha matumbo yao,"alisema Dkt. Kigwangala.

  Kwa upande mwingine, Dkt. Kigwangala alijitolea kuichangia shule hiyo msaada wa vitanda vyenye thamani ya sh. milioni tatu, kabati mbili kwa ajili ya chumba cha wanafunzi wasioona, na vifaa mbalimbali vya michezo.
   
 2. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,418
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Amesharudishiwa basitola yake?na kama anamuunga mkono zzk si ahamie cdm baada ya kukosa unec
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  KIGANGWALLA ni nani tena?? Nikumbusheni... Ah ni yule aliyekuwa anafanya kazi WAMA...

  Ohh aliyepewa UBUNGE toka IKULU,

  Oooh Nakumbuka alipeleka form kugombea CCM-NEC na Ki-BASTOLA...

  Oooh CCM Kamati Kuu wakalitupa JINA LAKE NJE; Na MWENYEKITI WA CCM TAIFA akasema wakitaka kuhama CHAMA
  na WAHAME!!! DUH, Sasa ya nini CHADEMA kaka... UMEFILISIKA KISIASA... ganga ya kwako!!!
   
 4. T

  Tewe JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  They are in the same boat. Simply Vibaraka tu hao
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Angejitolea mfano mwenyewe vipi bastola yake karejeshea.Hao wakuu wa shule hawakuzingatia usalama wa watoto lijamaa lina hasira sana.
   
 6. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Vijana, vijana, vijana Tanzania!!!! rudia kibwagizo x 100,000
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kingwangwala, who?
   
 8. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #8
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Zitto Zuberi Kabwe... The man himself! Mimi napenda kusoma tu vile wadau ambavo wanawaka moto na kutoa maneno ya hasira dhidi yake wakisikia huyu mkuu katamka kugombea.. Huwa natamani ningekuwa najua siasa kama wao (ambao wapo against) ili nielewe vipengele hivi.

  1. Hawapendi sababu anaungwa mkono na CCM wengi na maybe sababu inaonekana anapatana na baadhi kama vie Makamba Jr.? (Imagine Makamba Jr. katamka kua Zitto ni mwanasiasa ambae he is impressed by)
  2. Hawapendi sababu ni tishio kwa anayetazamiwa kugombea kwa chama hicho ambaye ni Mh. Dr. Slaa?
  3. Hawapendi sababu wanaona hafai na wala hana sifa za uongozi? AMA
  4. Hawapendi sababu ipi hasa? Kwanini watu wanachanganikiwa sana wakisikia Zitto in the lines of Presidency?

  Kama kuna mtu wa kujijibu hayo kwa kina na ufasaha nitashukuru saana.
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  inside story & fact.

  [​IMG] [​IMG]


  VIGOGO kadhaa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wametajwa "kuingilia" Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), MwanaHALISI limegundua.
  Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya idara hiyo zinaeleza kuwa vigogo hao wana mahusiano ya karibu na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe.
  Anayetajwa rasmi kuwa na mahusiano na Zitto ni Naibu Mkurugenzi wa TISS, Jack Zoka.
  Kufichuka kwa taarifa za kuwapo "uswahiba" kati ya Zoka na Zitto kumekuja katika kipindi ambacho CHADEMA kimekuwa kikituhumu maofisa wa juu wa usalama wa taifa kuvuruga uchaguzi mkuu uliopita.
  Aidha, kuibuka kwa tuhuma hizi kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuchapisha taarifa mbalimbali za mawasiliano kati ya Zitto na Rais Jakaya Kikwete.
  Baadhi ya mawasiliano hayo, ambayo Zitto ameyapeleka kwa rais, aliyapeleka pia kwa baadhi ya watuhumiwa ufisadi nchini.
  Kwa mujibu wa mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ambaye alitangazwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Kikwete; viongozi wa TISS walihusika, kwa kiasi kikubwa, katika kile alichoita, "Kuchakachua matokeo ya uchaguzi."
  MwanaHALISI limefanikiwa kupata rekodi ya mshororo wa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka.
  Kuna mwingiliano wa simu za mdomo na maandishi (sms) kutoka kwa Zitto kwenda kwa baadhi ya vigogo wa ngazi ya juu serikalini na TISS, hasa Zoka.

  Nyaraka za mawasiliano zinaonyesha kuwa Zitto amekuwa akiwasiliana na naibu mtendaji mkuu wa TISS huyo zaidi ya mara tatu kwa siku.
  Kwa mfano, Zitto na Zoka walifanya mawasiliano ya simu mara tisa hapo tarehe 8 Agosti. Simu iliyotumika katika mawasilino hayo, ni Na. +255756809535 ambayo hutumiwa na Zitto na +255754787550 ambayo hutumiwa na Zoka.
  Wakati mawasiliano hayo yanafanyika, Zitto alikuwa katika maeneo tofauti.
  Mawasiliano ya kwanza kati ya Zitto na Zoka yalipokuwa yanafanyika, simu ya Zitto ilisomeka kuwa alikuwa katika maeneo mbalimbali.
  Mathalani, wakati mwingine simu ilikuwa ikisomeka kuwa yuko Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam, Kigoma Urban (Mjini), Kigoma Rural (Vijijini), Mtwara, Uwanja wa ndege-Ilala, Oyster Bay, Ukonga, Upanga na katikati ya mji.
  Gazeti hili halikuweza kugundua mara moja undani wa mawasiliano ya Zitto na Zoka.
  Kinachofanya baadhi ya wachunguzi wa mambo kujenga shaka ni kwamba mmoja ni mwanasiasa, tena kutoka chama kilichopo nje ya utawala; na mwingine ni mtumishi wa idara ya usalama inayolalamikiwa kukandamiza upinzani nchini.
  Hata hivyo, taarifa zinaonyesha kuwa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka yalianza kupamba moto kuanzia tarehe 6 Agosti 2010, siku moja baada ya CHADEMA kuzindua kampeni zake za urais.
  Kulingana na uchunguzi, siku hiyo, tarehe 6 Agosti, simu ya Zitto ilisomeka kuwa yuko Kigoma Urban.
  Katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni, CHADEMA kupitia kada wake mashuhuri, Mabere Marando, iliibuka na lundo la tuhuma dhidi ya vigogo kadhaa wa serikali, CCM na idara ya usalama wa taifa.
  Akizungumza na maelfu ya wananchi katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, Marando alisema wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya Benki Kuu ya taifa (BoT), ulifanywa na serikali na washirika wake.
  Miongoni mwa vigogo aliodai kuwa walihusika kufanikisha wizi huo, ni rais wa sasa, Jakaya Kikwete, rais mstaafu Benjamin Mkapa, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Edward Lowassa.
  Akiongea kwa kujiamini, Marando alisema, "fedha za EPA ni wizi uliotiwa baraka na serikali ya CCM na ndio uliomsaidia rais Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005."
  Kuanzia hapo hadi sasa, Zitto na Zoka wamekuwa na mawasilino ya mara kwa mara, na karibu kila siku huzungumza kwa simu.
  Mawasiliano mengine ya mara kwa mara yalifanyika tarehe 7 Agosti 2010, siku mbili tangu hotuba kali ya Jangwani. Yalianza saa 10:17 na kuendelea tena saa 10:50, saa 10:51:31, saa 11:46:13, saa 12: 14:46, saa 12:26:48 na saa 13:50: 21.
  Lakini Zitto alipoulizwa kuhusu sababu ya yeye kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na vigogo wa TISS, alisema hajui na hakumbuki lolote kuhusu kuwapo mawasiliano hayo na Zoka au mkuu yeyote wa idara hiyo.

  Zitto amesema yeye, akiwa mwanasiasa na kiongozi, anazungumza na watu wengi kutoka katika taasisi na mashirika mbalimbali ndani na nje ya nchi, lakini hajui kitu kuhusu usalama wa taifa.

  Alipobanwa kuhusu mazungumzo yake na Zoka, hasa yale ya 3 Novemba 2010, saa nne na dakika 56 asubuhi, siku mbili baada ya uchaguzi kumalizika, Zitto alisema, "Siku hiyo nilizungumza na watu wengi sana. Siwakumbuki ni akina nani hasa."
  Alisema, "Hicho ndicho kipindi ambacho matokeo ya uchaguzi nchini kote yalikuwa yakizuiwa ikiwamo kwetu Kigoma. Na ukumbuke mimi nilipigwa mabomu na polisi na usalama wa taifa. Nakumbuka viongozi wengi wa vyombo vya ulinzi na usalama walinipigia simu kunijulia hali na kupata taarifa ya kilichotokea," anaeleza.

  "Sasa kama Zoka naye alinipigia siku hiyo sikumbuki; lakini nilipigiwa na wengi…Naomba uniambie kitu, hivi mnachokitafuta hasa ni nini?" aliuliza.
  Katika njia ya kujitetea, Zitto aliuliza, "Mwanasiasa kuongea na wakuu wa vyombo vya usalama ni kosa? Maana, hata kama ningekuwa nimezungumza naye, kosa langu liko wapi?" alieleza mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini.

  Alipoelezwa kuwa haoni hiyo ni hujuma dhidi ya chama chake kwa kuzungumza na viongozi wa TISS na kile ambacho amekuwa akikizungumza kikiwa hakifahamiki kwa viongozi wake, Zitto alisema, "Sijawahi kukihujumu chama changu mahali popote, siku yoyote."

  Jitihada za gazeti hili kuzungumza na Zoka hazikufanikiwa katika kipindi chote
  cha mwishoni mwa wiki, kwa vile kila alipopigiwa, simu yake ya mkononi ilikuwa haipokelewi.

  Hata ujumbe mfupi wa maneno uliotumwa kwenye simu yake saa 2:53 asubuhi ya Jumapili; ukieleza sababu za gazeti kuzungumza naye, haukujibiwa.

  Aidha, tarehe 2 Novemba, siku moja baada ya kuzungumza na Zitto, Zoka alinukuliwa akikana madai ya Dk. Slaa, kuwa TISS imesaidia kuvuruga uchaguzi.
  Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Zoka alisema, "Dk. Slaa amekuwa akidanganywa na watu wanaojiita maofisa wa usalama wa taifa."
  Hata hivyo, kuna meseji mbalimbali kuhusu udini na uamuzi wa CHADEMA kususia hotuba ya rais Kikwete ambazo zilitumwa na Zitto kwa baadhi ya wabunge wa CHADEMA ambazo zinadaiwa kuandaliwa na idara ya usalama wataifa.
  Ujumbe huo unadaiwa kuandaliwa kwa ustadi mkubwa katika kukuza suala la udini na kuleta mtafaruki katika chama.
   
 10. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Napita mbali si ana bastola ya kuwa tishia watu
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Hii ni moja ya mijadala inayoweza kujadiliwa Ijumaa usiku tu AshaDii.
   
 12. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  2005 wakati wa JK tulisemaga hivo hivo...atakua mkombozi wa watanzania, Rais handsome atapata kura nyingi za wanawake...haya...
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,609
  Likes Received: 2,001
  Trophy Points: 280
  Hizi shule badala zialike wageni rasmi ambao watatoa nasaha za kuwasaidia wanafunzi maisha yao ya uraiani,na jinsi ya kukabiliana na changamoto kutegemeana na either kama watatafuta ajira ama kuendelea na masomo ya juu,wao wanawaita wanasiasa njaa wenye kwenda kuzungumza pumba zao!
   
 14. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hiyo ya Kigwangwalla nimeipenda tena atakuwa kampeni meneja wake, watagawa vitumbua atakaekataa wanamtishia na Bistora Brigita tujiandae kula vitumbua.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #15
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  Kigwangala mzee wa vitumbua, press conference imeota mbawa? Au yale maamuzi magumu ndio yameota mbawa!
   
 16. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Zitto kugombea urais! You can't be serious. Kama anafaa basi ni kwa urais wa mdomoni lakini si urais wa nchi. Yeye bado anaishi kwenye mawazo ya ukigoma atatufanyia nini? Isitoshe ukiachia mbali kupata kismati cha kushabikiwa na vyombo vya habari, Zitto hana sifa hata moja ya urais. Anafaa kuwa mtumishi wa CCM au ISS chini ya bosi wake Zoka.
   
 17. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Matola, Hoja yako dhaifu,ila imepoteza mvuto zaidi ulipotaja gazeti la udaku la
  mwanahalisi!
  Mhariri wa mwanahalisi ni slaa!ulitegemea aandike nini?
  Nina kula ya zitto mkononi mwangu!
   
 18. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,817
  Likes Received: 36,921
  Trophy Points: 280
  Huyu Dr.Vitumbua si alisema anataka kuongea na waandishi wa habari mbona mpaka leo kimya???

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 19. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nachoshangazwa mimi ni kuwa kwa nini watu wengi ambao si Chadema wanaonekana kushupalia kumuunga mkono Zitto?!! Mfano huyu Hamis Andrea. Yaani katika hali ya kawaida uibuke umuunge mkono hivi hivi mtu ambaye atakuja kupambana na mtu ambaye chama chako kitamsimamisha? Iko namna hapa. Na ndio maana sishangai tuhuma kuwa Zitto anatumika. Wakina Hamis Andrea wanajua kabisa ndani ya Chadema hakuna utaratibu wa kutangaza nia katika ngazi ya Urais na ndio maana wanashadadia kitendo cha Zitto maana wangependa kuiona Chadema inakuwa kama CCM kwa kutengeneza makundi ya wataka Urais. Ndo maana navyoona tarumbeta za kina Hamis Andrea huwa natumia jicho la tatu kupata tafsiri ya wanachomaanisha.
   
 20. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ngoja nimsaidie Kigwangala kama Zitto atagombea urais basi mgombea mwenza awe Hussein Bashe.
   
Loading...