Naumwa kwa miaka mingi ila sizidiwi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naumwa kwa miaka mingi ila sizidiwi

Discussion in 'JF Doctor' started by ellyrehema, Jul 19, 2012.

 1. ellyrehema

  ellyrehema JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 1,047
  Likes Received: 693
  Trophy Points: 280
  Jamani habari zenu. kama kuna daktari ataweza kunisaidia tatizo langu hili nitafurahi sana. mimi nina miaka 34 na tangu nikiwa na umri wa miaka 24 nilianza kusikia kama maralia muda wote mara iningine ukipima inakuwepo ukinywa dawa hujisikii nafuu ila ukipima tena unakuta hakuna maralia, baadae nikaiona ni hali ya kawaida baada ya kuzoea. nahisi maumivu ya mifupa, masikio yanavuma ziiiiii!!!!, pia kichwa kinauma ila si sana. hali hii ni muda wote tangu nikiwa na umri huo. nimetumia dawa nyingi tu bila mafanikio. nilienda kwa watu wa tiba mbadala nikaambiwa eti mifupa yangu imezeeka kuliko umri wangu, pia nina sumu nyingi mwilini nahitaji kufanyiwa Detoxin, nilishindwa bei ya matibabu yao kwani niliambiwa laki tano. maisha yangu si mabaya na pia si mazuri saaana ni mtu wa kawaida kwani nina kipato cha wastani.na ninaishi kwa kufuata kanuni zote za afya.
  kinachonishangaza naugua sana kila mwezi lazima niugue maralia nilishapima ukimwi sina,
  SWALI je kuna hduma ya kuondoa sumu kitaalam(hospitalini?) na hii huduma inapatikana hospitali gani na kwa bei gani?. sasa naona nitakufa mapema na muda mwingine huwa naacha kunywa dawa tu na sizidiwi ila mwili wangu unaugua tu muda wote. naomba tuwasiliane kwa email yangu derick4u@ymail.com
   
 2. Lilian Masilago

  Lilian Masilago Verified User

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 246
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inwezekana kuna watakao kuja na majibu tofauti na yangu..well i agree to disaagree..
  USHAURI wangu...regardless imani yako...Nenda kaombewe kwa jina la Yesu na Uokoke(be carefull na manabii wa uongo)
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Badala ya wewe kumpa Ushauri wa kuombewa na wachungaji wewe unamuambia akaokoke? asipo okoka hawezi kupona? Pole sana kwa kuumwa ningelikushauri uende Hospitali kuu ya rufaa Muhimbili ukapime vipimo vyote mwilini mwako kisha uje utupe feedback wamesema nini huko Hospitalini? Kisha tutaweza namna ya kukusaidia pia waweza kuwasiliana na mimi email yangu Address ni hii hapa (fewgoodman@hotmail.com) pole sana bibie.@ellyrehema
   
 4. Lilian Masilago

  Lilian Masilago Verified User

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 246
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MziziMkavu,kuokoka ni zaidi ya kuombewa na wachungaji or anyone else.Kuokoka ni UPONYAJI wa mwili ,roho na nafsi....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Mimi mbona nimeokoka miaka mingi lakini bado ninaumwa roho na mwili? Unaweza kuokoka na bado ukaumwa mwili kuokoka kunatokana na roho sio mwili. mwili mbali na Roho ni mbali ni vitu 2 tofauti unawezakuokoka na bado ukawa unaumwa mwili upo pamoja na mimi mkuu Lilian Masilago?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  pole sana Ellyrehema.
   
 7. Lilian Masilago

  Lilian Masilago Verified User

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 246
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaweza kuwa unaumwa mwili(yes sometimes it happens) lakn sio roho (kama umeokoka kiukweli na sio kichina china)...otherwise tunaongea vitu tofauti kati yako na mimi. Nasema hivo kwa sababu roho yako ni ya muhimu zaidi na huu mwili utaishia kuwa mavumbi...
  Naomba nikupe ANGALIZO kuwa mwenye haki huwa anaishi kwa IMANI akisitasita Mungu hana furaha nae.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Usitie mambo ya Dini na Maradhi unaweza kuokoka unavyotaka wewe na maradhi ukawa nayo. Basi kusingekuwepo hospitali Duniani Watu wangelikuwa wanaokoka na kupona hata hao waliokufundisheni mambo ya kuokoka wanakwenda Ma Hospitalini acha imani yako ya kuokoka mpe Dawa huyu mgonjwa apone kisha ndio umwambie aokoke mkuu Samahani kama nitakukwaza na kuokoka kwako huko Lilian Masilago
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  duh,pole sana....
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  hatutaki pole tunataka mpe dawa au muombeekwa Mungu apone bi Neema hujambo lakini? Neema utafunga Ramadhani? neema?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. I

  Incredible JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 937
  Likes Received: 963
  Trophy Points: 180
  Nakushauri ukaombewe kwa jina la Yesu. Yesu anaponya watu wa dini zote tatizo ni sisi binadamu tunapenda kumfanya Yesu kama mali yetu binafsi.

  Ukiweza soma Biblia upade wa agano jipya na umwombe Yesu akuponye. Fanya hivyo mara kadhaa.
   
 12. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  yuko kny maumivu tumpe pole MziziMkavu,....kufunga mmmmmmmmh nitakuwa nakudanganya lol :redface:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  nahisi una tatizo la immunity...au lile la body kuattack immunity yako automatically.....i hope MziziMkavu hatakuambia utafute kwato la ng'ombe.....,lol:wacko:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Kwani kila kitu ni kwato la Ng'ombe bibie .. Neema? Kwato la Ng'ombe ni kwa ajili ya mtoto anaye kojoa kitandani sio kwato la Ng'ombe kwa kila maradhi upo pamoja bibie mpendwa?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  nakutania bwana,tupo pamoja,ila hio tiba ya kwato mmmmmmmmmmmmmnh mie siiamini,,,,,:wacko:
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Jaribu kwa mtoto anaye kojoa kitandani utapata majibu yake kisha unipe feedback Neema
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,135
  Likes Received: 2,158
  Trophy Points: 280
  Mkuu maneno yako wakati fulani yakupasa upime hilo jina kwa uzoefu wangu ni la kiume na sio sawa kumuita bibie...
  Kumshauri aende Muhimbili mmh! kwani mgomo mkubwa wa Madaktari ni vitendea kazi haswa mashine za kupimia n.k sidhani kama anaweza pata hivyo vipimo na akaja pona sawia kwa uzoefu mkubwa watu waendao muhimbili huambiwa wakafanye vipimo kwenye hospital binafsi na majibu wawaletee pale muhimbili na hii Madaktari wetu wliona ni kadhia iliyosababishga migomo
   
 18. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Siku za karibuni kuna huduma ya tiba mbadala maeneo mengi. Kwa wale wanaosikiliza vipindi hivyo kwenye radio hasa mtafahamu Praise power na WAPO radio zinatangaza kuhusu maeneo ambayo tiba hizo zinapatikana kule Kurasini, Mbezi Samaki na Kimara Stop Over. Huko hupimwa kwa computer na kubainisha kiwango cha sumu mwilini. Kisha huendesha zoezi la kuondoa sumu....bei yake ilikuwa Tz 20,000 (sijui siku hizi) na lazima kuingizwa kwenye mashine hiyo mara 3 ili kuhakikisha sumu imeondolowa mwilini. Kingine (hata kama mimi si daktari) maradhi kama hayo unayosema yanaweza kusababishwa na mionzi (rays) -ambazo sources zake zinafahamika au hazifahamiki. But try that one bibie
   
 19. M

  Mgalatia JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2012
  Joined: Nov 28, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nakushauri jitahidi kula matunda fresh kwa kuanzia tafuta beetroot moja na carrot moja utengeneze juice kila siku kwa siku tatu mfululizo unywe kila asubuhi kabla ya kula kitu na usile kitu mpaka baada ya nusu saa halafu uone. ushauri wa pili, nenda kwenye hospitali ya natural therapies opposite Hindu mandal hospital DSM waone uwaeleze ili wakufanyie kipimo cha mwili ( nadhani itakuwa bado shs 20,000) wanaweza kukusaidia sana. nazungumza kwa experience yangu ndogo.:cool2:
   
 20. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  nenda hospital, kamwelezee dk, atakupatia ushauri. yaweza kuwa myalgia, but lazima kutafuta sababu.!
   
Loading...