Nauli ya kwenda Marekani

I have collected flight cost data from across the web for travel from Dar Es Salaam to Washington, and have found the average flight price for this trip to be TZS 6,369,684

si kweli bali unategema na daraja unalopanda, hiyo ni bei ya daraja linaitwa bussines class, daraja la kawaida(economy class) kwa ndege za KLM ni dola 1,359 kwenda washington DC na majimbo hayatofautiani bei sana kwa economy class, KIbongo ni kama sh 2,853,900 tu.
 
Ingia site inaitwa skyscanner.net utajaza mwenyewe tarehe ya kusafiri, toka airport gani mpaka airport gani huko Marekani, itakupa list ya airlines zote zipigazo hiyo route, kila moja na nauli yake, masaa yote ya safari, utapitia wapi, n.k utapata mwanga.. Kumbuka nauli za ndege haziko fixed kama bus au treni, kuna factors nyingi zina determine bei ya nauli.
 
Kuwasaidia watu ni uungwana.

Mleta mada kama kweli hufahamu ulichouliza na unataka kujua, kwanza ufahamu unaenda likizo kwa gharama zako mwenyewe kuanzia nauli makazi ya kule visa na matumizi ukiwa kule.
Je ungependa uende USA kwa kusave hela yaani upunguze gharama pale inapowezekana au una fedha ya kutosha na hivyo gharama kwako sio kigezo?

Basi endelea kusoma maelezo ya Kasie shida yake tuu hawezi ku summarise naeleza kwa kirefuuu haya twende....

Kama utataka kuwa likizo USA kwa gharama nafuu basi anza na kubook ticket yako mapema kupitia tovuti za makampuni ya ndege na usipitie kwa travel agent. Kumbuka travel agent atakuchaji gharama ya kukukatia ticket. Kuna airlines ambazo bei zake ni nafuu wewe tumia mtandao kiufasaha ila hapo kwenye nafuu uwe makini maana nyingine zaweza kukuletea shida wakakukatia ticket ya waiting list maana yake ukikuta ndege haina abiria wengi siku hiyo utaenda ila ukikuta abiria waliokata ni wengi basi wewe na nafuu unawekewa waiting list na unaweza kuachwa. Mfano tangu mwezi wa tatu Emirates walikuwa na ofa na ticket zao zilikuwa chini sana, huo ulikuwa sio msimu wa abiria. Ukiwa na lengo la kusave hasa kwenye nauli likizo yako waweza ipangilia msimu ambao airlines hazina wateja yaani low customers season, hapo ndo airlines nyingi hutoa ofa na hushusha bei ya ticket zake.

Kwa upande wa mahali pa kufikia basi unagoogle cheap hotels in USA na u specify mji utakao fikia. Hapo utapata list ya hotels au lodge na watakupa na bei zake. Ziko za kulipia kabla na ziko za kulipia baada ya kufika ila booking yako inaheqhimiwa. Pia waweza uliza hotel uliyobook wakakupokea airport yaani airport peak up na watakuchaji kutokana na gharama zao. Utaona hotel nyingine wanatoa ofa ukibook hotel yao wanatoa ofa ya kukupokea airport na siku unayoondoka pia wanakupeleka.
Pia kama utakuwa mpenda adventure kama Kasie yaani napenda kujua vitu kwa kujifunza na usiwe muoga basi utagoogle means of transport from airport to the hotel ambayo umebook. Hapo utaletewa njia mbali mbali kuanzia public transport hadi taxi au magari ya kukodi kama huku yale tunaita rent a car.

Kwa uzoefu wangu wa kuzurula mie huwa napenda kujifunza maana najua kule ni ugenini hivo kupokelewa na kupelekwa mahali kama nursery school student naona kama niko jela. Huwa nachukua train from airport to city centre kisha nachukua public transport to near the hotel. Kama hotel niliyo book daladala hazifiki hapo basi hapo nnaposhuka hadi kwenye hotel kama ni walking distance ntatembea ila tuu kama sina mizigo. Maana Kasie nasafirigi na begi moja tuu tena lile la size ya kati hivo ni rahisi kulikokota ukiwa unatembea maana kwa wenzetu miundombinu safi. Na kama bado pana umbali basi ntachukua taxi.

Note hii itafaa iwapo huko unakofikia iwe muda wa kuanzia asubuhi hadi jioni ya saa 10. Giza likishaingia au iwapo unawasili usiku basi haina mantiki kutumia public transpory maana u mgeni ni vema ukatumia usafiri wa kupokelewa. Lengo langu kutumia public transport na kutembea sio kusave ila kujua kujifunza kuona mji na kufurahia maana napenda hivyo. Pia uzingatie hali ya hewa ya msimu unaoenda huko. Usijetumia njia hii msimu wa winter kali au mvua kali hautaeleweka.


Kitu kingine cha kuzingatia ni maeneo mazuri ya kutembelea ambayo utayafurahia. Google attractive visiting areas near to the hotel au within the city you'll be visiting. Hapa waweza tumia travel agent na ukaenda watakupangia ratiba na gharama na ukalipa ukishafika huko. La waweza kuwa unazunguka kwenye malls tuu na kushangaa magorofa na fly over.

Mwisho wa yote ukiona huo ji usumbufu na hapendi adventure kama Kasie basi tumia travel agent watakufanyia kila kitu na utakuwa unaendeshwa na kupelekwa kama mzigo.

All the best, feel free to ask any question. Enjoy your leave, with plans it's gonna be perfect.

Kasie.
 
Back
Top Bottom