Kwa sasa nauli ni dollar 100,mabasi ni ratico na classic na unaweza kukosa siti kwa sababu hua wana pakia mizigo kwa wingi sana inaenda Lubumbashi,pia passport, Chet cha COVID,Chet cha manjano dollar 50 ya Visa kuingia Congo ila Zambia ni bule,lakini pale mpakani kuna siku hua kuna watu wa uhamiaji wana weza kutaka uwape hata dollar 10,kwa hiyo nayo ni yakuweka kwenye bajeti maana wana tafta tu kasababu kadogo usipo wapa una weza kuachwa na gari nazani mpaka hapo utakua umepata mwanga.
Nb. Congo sio inchi ya kutaftia maisha maana amani ni ziro mda wowote tu kina waka,hata raia wana roho mbaya police na wana jeshi wote wana penda kuomba omba sana pesa kama huna wanaweza kukuumiza,maana wana tembea na siraha za moto mda wote na bange wanavuta bila woga na waningia baa na siraha wanalewa fikiria zaidi kabla hujainza safari,maana una weza fanikiwa kufika ila ukajuta zaidi.