Hebu angalia hawa jamaa wameshatutoa kwenye hoja ya msingi na sasa wanatusahaulisha kwa kutuletea hizi hoja zisizo na mashiko kama ya nauli.Wakala wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam ( DART ) ambao watatoa huduma ya usafiri wa umma katika njia na miundombinu ya DART katika kipindi cha mpito wamependekeza viwango vipya vya nauli kama ifuatavyo;
Kabla ya kufikia uamuzi wa kurudhia viwango hivyo vipya vya nauli, SUMATRA imeandaa mkutano ili kupokea maoni toka kwa wadau mbalimbali utakaofanyika September 15 , ukumbi wa Karimjee, DSM kuanzia saa 3 asubuhi. Wote mnakaribishwa.
Nashangaa na wanaposema kuwa wanafunzi watalipa NUSU ya nauli ya watu wazima! -- sh 250, 350, 400, 450 (Wanafunzi?)kutoa hizi nauli wamezingatia vigezo gani ?
na tatizo na uwezo wa kufikiri wa viongozi wetu aiseeeNashangaa na wanaposema kuwa wanafunzi watalipa NUSU ya nauli ya watu wazima! -- sh 250, 350, 400, 450 (Wanafunzi?)
Hii nauli ni kubwa kuzingatia hali ya maisha ya Mtanzania na viwango vya mishahara! Bora wangeacha nauli ibaki km ikivyokuwa awali!
Mkombozi anapokuwa mwizi tufanyeje?