Kwenda moshi ni lazima ulipishwe nauli ya arusha pia inategemea na basi husika ila nauli ipo kwa viwango
Kuna Ordinary nauli ni 23000/= = haya ndo yale mabasi gonga nyundo na seat ni 3 by 2 unaeza kukuta lina tv moja au 2 au zisifanye kazi hakuna cha bure kama pipi soda wala keki hapo safari tuu na hayanaga muda muhafaka au zikafanya hili ndo daraja la kawaida
Semi luxury 33000 = Hili ndo daraja la kati hapa ndio kampuni nyingi zinatumia unakuta bus lina tv mbili na kuendelea seats ni 2 by 2 wanagawa vinywaji pia na pipi na biscut au cake kwa baadhi pia Ac zipo zenye nazo na zisizo nazo kwani kwao sio lazima.
Luxury / VIP 36000 - 46000/= luxury hapa gari zake huwa hazina tofauti sana na semi ila kuna vitu huwa vinaongzwa kama tv ni 5 na kuendelea na lazima liwe na choo
VIP bus linaweza lisiwe na choo ila ni mlolongo wa seat huwa ni 2 by 1.