Malungwana
Senior Member
- Sep 14, 2013
- 187
- 99
Habari wan jamvi.
Usafiri wa baharini kati ya Zanzibar na Dar es salaam, umeboreshwa sana na boat nzuri sana za Bakharesa, boat zao ni nzuri sana na zimesaidia sana.
Tatizo linalojitokeza kwa sasa ni ulanguzi wa tiketi, na ulanguzi huu ungekua unafanyika na madalali wa nje (middlemen) hapo tungesema mengine, lakini ulanguzi unafanyika ndani kabisa katika ofisi, (ndani kwa mkatisha tickets), nitatoa mfano ulio hai kabisa kwa ndugu yangu ambae nilikua nasafiri nae kutoka Dar kwenda Zanzibar, siku ya tarehe 8 May, mimi nilikua nina ticket number kwa sababu nilishalipa in advance, mwenzangu alikua yeye anataka kukata ticket palepale ofisini bandarini,tulipofika akaambiwa ticket zipo ila ni Tsh 50,000 kutoka Dar - ZNZ, kwa sababu ya haraka na ulazima wa safari, ikabidi alipe, lakini cha ajabu ticket ilipotolewa imeandikwa Tsh 25,000, ikawa ni kelele sana, na tukataka tutafute wakutusaidia, lakini haikuwezekana kabisa, ticket za boat hua ni Tsh 50,000 kwa watanzania kama ni VIP seat, lakini kalipa Tsh 50,000 halafu akapewa ticket ya Economy class......huu ni wizi wa waziwazi kabisa, na inakera sana.
Kuna watu wengine walikua wanakuja na hio Tsh 25,000 tu na wanaambiwa tiket ni elf 50, na hawana nyengine,yaani unawaona wanaishiwa nguvu kabisa, hadi unawaonea huruma.
Nauliza hvi vyombo vinavyohusika na udhibiti wa nauli hawajui haya yanayotendeka??? au wako pamoja na hao walanguzi???
Naomba kuwakilisha.