MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,760
- 48,408
Shukran wadau kwa rambirambi zote mlizotupa, binafsi nimepokea nyingi tu kwenye Whatsapp kutoka kwa washkaji ukanda huu, ni dhahiri likija suala la magaidi Afrika mashariki huungana na kuwa wamoja. Hawa watu hawana mipaka, ni mazombi yaliyozaliwa kwa bahati mbaya, yameaminishwa mambo ya kiajabu ajabu, na nia yao huwa kueneza uwoga, ila wakiona jamii inaungana kwa ujasiri na kuwa wamoja dhidi yao, wanahesabu kama hasara kubwa sana.
Hivyo binafsi natoa shukrani kwa majirani wote waliotutumia rambirambi, lakini pia kwa wale kizazi cha nyoka Watanzania wachache waliokesha humu JF wakibeza na kuchekea mauaji yaliyokua yanaendelea, nawapa zoezi rahisi sana, nenda kajiangalie kwenye kioo kwa zaidi ya dakika kumi, ujiulize huyo mtu aliye ndani ya hicho kioo anakutazama, kama ndiye ulikusudia kuishi naye kwa miaka yote ijayo, au anahitaji kurekebisha kitu.
Utani wetu ubaki kwenye mitandao, lakini likija suala linalogusa uti wa mgongo wa jamii yetu, tunafaa kulikemea sote kwa pamoja, ifahamike hii mipaka imechorwa na mzungu na kutupa majina ya kutumia kwenye utaifa.