Natarajia kuokoka

bachelor sugu

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
2,689
Reaction score
3,651
Habari za jioni wapendwa katika bwana,

Sawa na mada tajwa hapo juu,imefika muda sasa nafikiria KUOKOKA yaani kuwa mtu wa tofauti na nilivyokuwa hapo awali.

Nimejifunza mengi sana kwa kuwemo humu JF tangu nilipokuwa natembelea Forums kama mgeni mpaka nilipojiunga rasmi,kiukweli kuna mengi nimejifunza mazuri na mabaya na bado pia naendelea na nitaendelea kujifunza.

Nina mpango wa KUOKOKA kwa kuacha yale yote ambayo kwa namna moja ama nyingine yaweza kuwa yanawakwaza wengine kama vile
Matusi
Lugha chafu
Majibu ya mkato yenye kukwaza
Kejeli n.k

Pia ninatarajia siku ya huo wokovu kuacha kuchangia wala kusoma thread za siasa hasa za wana LUMUMBA a.k.a Wasaka vyeo ambao kwa hakika huwa ni watu wanaoniumiza roho yangu maana wao huona poa tu hata pale yanapofanyika yale ambayo ni kinyume na utu na mazoea yetu sie watanzania ila wao hukenua meno na kushangilia.

Tafadhali naomba msaada wenu katika kukamilisha huu wokovu wangu basi niunge mkono kwa KUTONIKWAZA kwa kufanya yale ambayo nimeahidi kutowafanyia nyie wenzangu.

Wenyeji katika majukwaa ya
Biashara,uchumi na ujasiriamali
Kilimo,ufugaji na uvuvi
Mchezo na burudani
Na mengineyo yasiyo na mfungamano wa kisiasa naombeni mnipokee nitakuwa nikilala huko ili nipate SITI YA KUDUMU kama wale ndugu zangu wanaolala kwenye Ule UZI WA KUPEANA LIKES.

Nawatakieni usiku mwema na Poleni kwa Starehe ndugu zangu.

Sincerely,Bachelor Sugu.
 
Hahahaha una pepo mkuu hataki hata uandike vizuri ona uzi ulivoandika kinjogi njogi
Mkuu sio kinjogi njogi bhana simu iliteleza halafu sikuweza kuona but mods watatimiza jukumu lao.
 
Kuokoka ni maamuzi magumu na ambayo hayahitaji mjadala na wanadamu, fanya unavyoitwa moyoni, usisikie wala kumwamini mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…